Kupitia filosofia hii
utapatikana ushauri kwamba wazo likisaidiwa na shauku kubwa lina tabia ya kujigeuza lenyewe kuwa katika kitu chake
halisi. Kabla ya kumalizia ningetamani kukuachia mapendekezo kwamba mtu anaweza
akakuta kwenye simulizi hii, na katika simulizi ya kuundwa kwa Shirika la chuma
cha pua la Marekani(United States Steel Corporation), maelezo kamili ya njia
ambayo wazo hufanya badiliko la kushangaza.
Katika utafiti wako wa siri
ya njia hii, usitegemee muujiza kwa sababu hautaupata. Utapata tu sheria za
milele za Asili. Sheria hizi zipo kwa kila mtu mwenye Imani na Ujasiri wa kuitumia. Zinaweza kutumika kuleta uhuru kwa
Taifa au kuleta utajiri. Hakuna gharama kuokoa muda unaohitajika kuzielewa na
kuzishika.
Wale wanaofikia maamuzi mara
moja na kufahamu wazi ni nini wanachotaka, na kwa ujumla hukipata. Viongozi
katika kila nyanja ya kimaisha huamua haraka na kwa uthabiti. Hiyo ndiyo sababu
kubwa kwanini ni viongozi. Dunia ina tabia ya kuweka nafasi kwaajili ya watu
ambao maneno yao na vitendo huonyesha wanafahamu ni wapi wanakokwenda. Kutokuwa
na uamuzi ni tabia ambayo kwa kawaida huanzia ujanani. Tabia hukomaa kwa kadiri
ujana unavyokwenda kupitia shuleni na hata kupitia Chuo Kikuu au Chuo bila ya
kuwa na ukamilifu wa lengo. Udhaifu
mkubwa wa mifumo yote ya elimu ni kwamba hawafundishi watu kusisitiza tabia ya maamuzi kamili.
Lingekuwa ni jambo la faida
ikiwa kungekuwa hamna Chuo kikuu au chuo ambacho kingeruhusu udahili wa
mwanafunzi yeyote mpaka aweze kutamka malengo yake makubwa ya kumaliza masomo
ni yapi. Ingelikuwa bado ni jambo lenye faida kubwa zaidi ikiwa kila mwanafunzi
anayeanza shule angelazimishwa kukubali mafunzo katika mtindo wa maamuzi, na kulazimishwa kufaulu mtihani wa ridhaa katika
somo hili kabla ya kumruhusu kuendelea.
Tabia ya kukosa uamuzi
ilishikwa kwa sababu ya mapungufu ya mifumo ya mashule yetu kuwapeleka
wanafunzi kwenye fani wanazochagua, ikiwa kweli wanachagua fani zao. Kwa ujumla
vijana ambao ndio wanatoka kumaliza shule hufanya kazi yeyote inayoweza
kupatikana. Wanachukua nafasi ya kwanza wanayopata kwasababu wameangukia katika
tabia ya kutokuwa na uamuzi. Watu tisini na nane kati ya kila watu mia moja
wanaofanya kazi ya kuajiriwa leo wapo katika nafasi wanazoshikilia kwasababu
walikosa ukamilifu wa maamuzi ya kupanga nafasi kamili, na maarifa ya jinsi ya
kuchagua mwajiri.
Ukamilifu wa maamuzi mara nyingi huhitaji ujasiri, wakati
mwingine ujasiri mkubwa sana. Watu 56 waliosaini tangazo la uhuru waliweka
rehani maisha yao katika uamuzi wa kubandika saini zao kwenye lile tamko. Watu
wanaofikia uamuzi kamili kujipatia kazi fulani na kufanya maisha yalipe gharama
wanayoomba hawatahatarisha maisha yao katika uamuzi huo, wanahatarisha uhuru wao wa kiuchumi .
Uhuru wa kifedha, utajiri,
biashara nzuri na nafasi za ajira hazipo ndani ya uwezo wa kuzifikia kwa mtu
anayepuuzia au kukataa kutegemea kupanga na kuvidai vitu hivi. Mtu anayetamani
utajiri katika roho ileile Samuel Adams aliyotamani Uhuru wa Makoloni ana
uhakika wa kupata utajiri.
Katika Sura ya 7 ya Mpango
madhubuti utakuta maelezo kamili kwa ajili ya kutafuta soko la kila aina ya
huduma. Utapata pia maelezo ya kina juu ya kuchagua mwajiri unayemtaka na kazi
unayotamani. Maelekezo haya yatakuwa hayana thamani kwako ikiwa kama HUTAAMUA
MARA MOJA kuyaweka katika mpango wa kivitendo.
Leo tumemaliza sura ya 8 ya kitabu hiki Fikiri Utajirike au Think & Grow Rich, Alhamisi tukutane tena kwa Sura mpya ta 9
...............................................................
Leo tumemaliza sura ya 8 ya kitabu hiki Fikiri Utajirike au Think & Grow Rich, Alhamisi tukutane tena kwa Sura mpya ta 9
...............................................................
*Semina yetu ya Michanganuo ya biashara inaendelea katika group la whatsapp la MICHANGANUO ONLINE, email na private blog kwa kiingilio cha sh. elfu 10. Masomo ni kila siku usiku saa 3. Ofa mbalimbali vikiwemo vitabu, templates na masomo ya semina zote zilizopita. kUJIUNGA tuma ujumbe wa wasap kwa namba 0765553030 au bonyeza link, https://chat.whatsapp.com/KO79AIJZOMVHBY2SlDdJBC
Kwa vitabu fungua; SMART BOOKS TANZANIA.
Kwa vitabu fungua; SMART BOOKS TANZANIA.
0 Response to "UHURU KIFEDHA, UTAJIRI, BIASHARA NA AJIRA NZURI VIPO KWA YULE ANAYEPANGA NA KUVIDAI"
Post a Comment