Leo ni siku ya kwaza ya mwezi wa tano May
mosi, ni siku ya kwanza ya muda wamaisha yetu yaliyobakia hapa duniani. Kwa
wafanyakazi katika sekta mbalimbali ni siku ya kutafakari na kujiuliza ikiwa ni
kitu gani hasa wanachohitaji bila kujihukumu na mazingira ama hali yako ya huko
nyuma ulikotoka.
Inawezekana huko nyuma mambo yako hayakuwa mazuri hata kidogo au
yalikuwa mazuri lakini huu si wakati wa kutathmini malengo yako au ndoto zako
kwa kutazama huko nyuma ilikuwaje ni wakati wa kuyatazama upya malengo yako
ukizingatia tu kile unachokitaka maishani, ukitafutie maarifa, urekebishe upya
mpango wako na mwisho upate mafanikio makubwa, makubwa ambayo hujawahi hata
siku moja kuwa nayo katika maisha yako yote huko ulikotoka.
Kwa imani, kauli na fikra chanya muda wote mwili wako
utafanya kile kile ambacho akili yako imekuwa ikiuambia mara kwa mara kwa kujua
au hata kwa kutokujua. Ikiwa tunataka mafanikio chanya kifedha na kimaisha kwa
ujumla katika maisha yetu, hatuna budi kuzuia na kuondoa kabisa mambo yote hasi
yanayotuzunguka iwe ni katika vitu vinavyotuzunguka, watu na hata mawazo yetu
wenyewe kwani chochote kile tunachoelekezea nguvu na akili zetu kiwe kibaya au
kizuri, akili zetu hukibadilisha kuwa katika kitu halisi tuwe tunapenda au
hatupendi.
Lenga tu katika ndoto na malengo yako na jiweke mbali
kabisa na vitu, watu na matukio yenye mlengo hasi yanayoweza kukufanya kutoa
pia kauli hasi, hii inaweza ikawa vigumu sana kutekeleza hasa katika nyakati
hizi zilizojaa kila aina ya taarifa lakini inawezekana ikiwa utaamua kufanya
maamuzi. Wewe mwenyewe ndiye uliye na uamuzi wa mwisho wa kuruhusu taarifa au mawazo
yeyote yale kutoka nje kuingia akilini mwako, hata ikiwa kuna watu wako wa
karibu vipi ambao unahisi wanakutoa katika mstari wa malengo yako una uwezo na
haki ya kuwaambia “jamani naombeni mkae mbali na mimi nitimize kwanza malengo
yangu.” Jihusishe tu na vitu au watu walio na mawazo ya kujenga ikiwa kama
kweli umeamua kubadilika.
Achana kabisa na kauli kama vile, “siwezi”, “ni ngumu mno”
“haiwezekani” na “sitaweza” kauli kama hizi zitajijenga katika akili yako na
kushika mizizi kama vile magugu yafanyavyo katika shamba la ngano safi
zikijifanya kuwa nazo ni safi kumbe ni vitu viharibifu. Kauli hizi zikizoeshwa
akilini mtu hujikuta akirudiarudia makosa yaleyale aliyokuwa akiyafanya zamani.
Iwe wewe ni mfanyakazi au hata unafanya shughuli zako za
kujiajiri, kila mtu ana ndoto zake, hizo ni njia tu za kuzifikia ndoto hizo.
Jambo jingine la kuzingatia ni kwamba binadamu hatujaumbwa kudumu na kitu
kimoja maisha yetu yote, aliye kwenye ajira leo itafika muda unaweza ukaja
kumkuta amebadilika na kuwa mfanyabiashara mkubwa au mwekezaji. Hali ni hivyo
hivyo ilivyo kwa waliojiajiri au wenye biashara zao binafsi, kesho na
keshokutwa unaweza kuja kumkuta mtu aliyekuwa na biashara zake akifanya kazi
kwa mtu katika kampuni. Hivyo binafsi siamini kama kuajiriwa ni laana hata
kidogo bali ni njia bora ya kuelekea kujiajiri
Ajira na kujiajiri ni vitu 2 vinavyotegemeana na hakuna
kilichokuwa bora kushinda mwenzake, ikiwa kila mtu angeamua kuwa na biashara
yake au kampuni, wafanyakazi wangetoka wapi? Lakini kitu cha kuzingatia hapa ni
malengo yako katika kile unachokifanya sasa iwe umeajiriwa au umeajiri. Ikiwa
ndoto zako ni siku moja kuja kuajiri kumiliki biashara unaweza ukaanza na
kuajiriwa kwanza wala siyo kosa hata kidogo, halafu mwishowe ukaja kugeuka
kuajiri watu wengine na wewe.
SOMA: Hivi unajua kila binadamu ni lazima afanye biashara angalao mara moja katika maisha yake yote?
Hivyo ndivyo mzunguko ulivyo duniani kote. Mtu yeyote
asije akakudanganya kwamba eti ajira au kufanya kazi ya mtu mwingine au
serikali ni jambo baya, ni utumwa nk. hapana, hiyo ni njia tu ya wewe kufikia
ndoto zako, na kukamilisha mzunguko ambao ikiwa kama usingekuwepo basi mambo
yasingelikwenda kabisa duniani, ni sawa kama ilivyokuwa katika mbuga ya
wanyama, Simba na chui wapo lakini ni lazima pia kuwe na nyasi, miti, swala,
nyati na pundamilia ili simba chui na wanyama wengine wote hao waweze kuishi,
ukiondoa kimoja hakuna mbuga ya wanyama tena.
……………………………………………………
Ndugu msomaji, vitabu 3 vya self help books Tanzania vipo
na unaweza ukajipatia nakala yako katika mifumo yote miwili iwe unataka
softcopy kwa njia ya email au hardcopy kitabu halisi cha karatasi. Softcopy
tunatuma kwa njia ya email na hardcopy tunakuletea mpaka ulipo ikiwa upo Dar es
salaam. Mikoani tunatuma kwa mabasi au unaweza kumuagiza mtu anayekuja Dar.
Tazama majalada yake hapo chini pamoja bei zake.
Kwa anayenunua softcopy ya kitabu cha MICHANGANUO YA
BIASHARA NA UJASIRIAMALI anapata pia na offa ya kujiunga na group la masomo ya
kila siku WHATSAP pamoja na masomo mbalimbali na semina zilizopita.
Usisahau pia katika Group la WHATSAPP masomo ni kila siku kwa mfano leo Jumatatu tutakuwa na somo lisemalo, "HATUA 3 MUHIMU UNAZOWEZA KUZIDHARAU LAKINI UKIZICHUKUA NI LAZIMA MIPANGO YAKO IZAE MATUNDA" Pia Tafsiri ya kitabu cha Think & Grow rich nayo itakuwepo na leo ni sehemu ya 3 ya sura ya 10
Usisahau pia katika Group la WHATSAPP masomo ni kila siku kwa mfano leo Jumatatu tutakuwa na somo lisemalo, "HATUA 3 MUHIMU UNAZOWEZA KUZIDHARAU LAKINI UKIZICHUKUA NI LAZIMA MIPANGO YAKO IZAE MATUNDA" Pia Tafsiri ya kitabu cha Think & Grow rich nayo itakuwepo na leo ni sehemu ya 3 ya sura ya 10
SIMU: 0712202244,
WHATSAPP: 0765553030
SOFTCOPY KWA EMAIL SH. 10,000
HARDCOPY DAR NI SH. 22,000
SOFTCOPY KWA EMAIL SH. 5,000
HARDCOPY DAR NI SH. 10,000
SOFTCOPY KWA EMAIL SH. 3,000
HARDCOPY DAR NI SH. 5,000
0 Response to "SIKU YA MEI MOSI: JE AJIRA NI JAMBO BAYA, UTUMWA NA KUKOSA MALENGO? "
Post a Comment