Dalili
za Ukosefu wa Uvumilivu
Hapa utakuta adui wa kweli wanaosimama
katikati yako na mafanikio ya maana. Hapa hautakutana tu na dalili
zinazoonyesha mapungufu ya msimamo, bali pia sababu za ndani kabisa katika
ufahamu wa ndani za udhaifu huu. Isome orodha kwa uangalifu na ukubali mwenyewe
kwa uaminifu KAMA KWELI UNATAKA KUFAHAMU WEWE NI NANI NA NI NINI UNACHOWEZA
KUKIFANYA. Haya ni madhaifu ambayo ni lazima yadhibitiwe na wale wote
wanaotafuta utajiri.
1. Kushindwa
kutambua na kuelezea kwa ufasaha hasa kile unachotaka.
2. Kuahirisha
kwa sababu au bila sababu(mara nyingi kukisaidiwa na jeshi la kutisha la
visingizio na udhuru)
3. Kukosa
moyo wa kujifunza ujuzi maalumu
4. Kukosa
uamuzi, “tabia ya kukwepa wajibu” katika matukio yote badala ya kukabiliana na
mambo kwa ukweli (pia kukisaidiwa na visingizio)
5. Tabia
ya kutegemea visingizio badala ya mipango kamili kwa ajili ya kutatua matatizo
6. Kuridhika
binafsi. Ipo dawa lakini kidogo sana kwa ajili ya tabia hii na hakuna matumaini
kwa wale wanaosumbuliwa nayo.
7. Kutokujali,
kwa kawaida huakisiwa katika utayari wako wa kukubaliana katika matukio yote,
kuliko kukutana na upinzani na kupambana nao.
8. Tabia
ya kuwalaumu wengine kwa makosa yako na kukubali mazingira yasiyofaa kama
kwamba hayaepukiki.
9. Udhaifu
katika shauku unaotokana na kutokujali kwenye uchaguzi wa sababu zinazochochea
vitendo.
10.
Utayari hata wa hamu ya kujitoa katika dalili
za mwanzo za kushindwa (kunakotegemea moja au zaidi ya hofu sita za msingi)
11.
Ukosefu wa mipango iliyoratibiwa, kuwekwa katika maandishi ambapo inaweza
ikachanganuliwa.
12.
Tabia ya kupuuzia kusogelea mawazo au kudaka
fursa wakati inapojitokeza yenyewe.
13.
Kutamani
badala ya kudhamiria.
14.
Tabia ya kukubaliana na umasikini badala ya
kulenga katika utajiri – ukosefu wa jumla wa shauku ya kuwa, kutenda na kumiliki.
15.
Kutafuta aina zote za njia za mkato za kupata
utajiri, kujaribu kupata pasipo kutoa
kiasi kinacholingana, mara nyingi huakisiwa katika tabia ya kucheza kamari au
jitihada za kufanya majadiliano ‘makali’ ya bei.
16.
Hofu
ya kukosolewa, kushindwa kutengeneza mipango na kuiweka
katika vitendo kwa sababu ya kile watu wengine wanachofikiria kufanya au
kusema. Adui huyu hukaa mwanzoni mwa orodha, kwa sababu hukaa kwa ujumla katika
akili ya ndani pasipo kushitukiwa (tazama hofu sita za msingi katika Sura ya
15)
Hebu tuzikague baadhi ya dalili za hofu ya
kukosolewa. Wengi wa watu huruhusu ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla
kuwaathiri kiasi kwamba hawawezi kuishi maisha yao kwa sababu huogopa
kukosolewa.
Idadi kubwa ya watu hufanya makosa kwenye
ndoa, hutimiza makubaliano na kuingia maisha ya mateso na huzuni kwasababu wanahofia ukosoaji unaoweza kufuata
ikiwa watarekebisha makosa (Mtu yeyote aliyejiweka chini ya aia hii ya hofu
anafahamu uharibifu usiorekebishika inaoufanya kwa kuharibu malengo,
kujitegemea na shauku ya kufanikiwa)
Mamilioni ya watu hudharau kupata elimu ya
ziada baada ya kuwa wamemaliza shule kwasababu wanahofia ukosoaji. Idadi
isiyohesabika ya wanaume na wanawake wote wadogo kwa wakubwa huruhusu ndugu
kuharibu maisha yao kwa kisingizio cha wajibu kwa sababu huogopa ukosoaji
(wajibu haumhitaji mtu yeyote kujisalimisha katika uharibifu wa malengo yao
binafsi na haki ya kuishi maisha yao katika njia zao wenyewe)
Watu hukataa kuchukua hatari kwenye biashara
kwa sababu wanaogopa ukosoaji unaoweza kufuata ikiwa watafeli. Woga wa ukosoaji
katika mambo hayo una nguvu kuliko shauku
ya mafanikio. Watu wengi sana hukataa kujiwekea malengo makubwa, au hata
kupuuzia kuchagua ajira kwasababu wanahofia ukosoaji wa ndugu na marafiki
wanaoweza kusema, “usiwe na malengo makubwa hivyo watu watafikiria
umechanganyikiwa”
Wakati Andrew Carnegie alipopendekeza kwamba,
nijitolee miaka 20 kwa ajili ya ukusanyaji wa falsafa ya mafanikio ya mtu,
msukumo wangu wa kwanza wa fikra ulikuwa ni hofu ya kitu gani watu wangeweza kusema.
Pendekezo liliweka lengo kwa ajili yangu lisilolingana kabisa na lengo jingine
lolote nililowahi kuwa nalo. Kwa haraka kama mwanga wa tochi, akili yangu
ilianza kujenga visingizio na sababu, zote zikiwa na dalili za hofu ya asili ya
ukosoaji.
Kitu ndani yangu kilikiniambia, “Hautaweza
kuifanya- kazi hiyo ni kubwa mno na inahitaji muda mwingi mno – ndugu zako
watakufikiriaje? Utaendeshaje maisha yako?
Hakuna mtu aliyewahi kuanzisha falsafa ya
mafanikio hivyo unayo haki gani ya kuamini unaweza kufanya? Wewe ni nani kwa
vyovyote kuwa na malengo makubwa kiasi
hicho? Kumbuka kuzaliwa kwako masikini. Unaelewa nini kuhusu falsafa? Watu
watafikiri umechanganyikiwa akili(na walifanya hivyo). Kwanini watu wengine
hawajawahi kufanya hivi kabla ya sasa?”
Haya na maswali mengine mengi yalimulika
katika akili yangu na kutaka majibu. Ilionekana kama kwamba Dunia yote ilikuwa
imenigeukia ghafla kwa lengo la
kunidhihaki ili niachane na shauku yote ya kutekeleza pendekezo la Bwana
Carnegie. Nilikuwa na fursa iliyokuwa wazi muda uleule ya kuiua nia kabla
haijaniongoza.
0 Response to "IKIWA KWELI UNATAKA MAFANIKIO, UDHAIFU HUU NI LAZIMA UUKWEPE"
Post a Comment