UFAHAMU WA PESA NI LAZIMA UJENGWE KWA KUTAKA ISIPOKUWA LABDA MTU AZALIWE NAO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UFAHAMU WA PESA NI LAZIMA UJENGWE KWA KUTAKA ISIPOKUWA LABDA MTU AZALIWE NAO

FIKIRI UTAJIRIKE SURA YA 9 SEHEMU YA II

Ufahamu wa umasikini hujengeka pasipo mtu kutumia kwa hiyari tabia zinazoendana nao. Ufahamu wa pesa ni lazima ujengwe kwa kutaka isipokuwa tu labda mtu azaliwe nao.


Shika umuhimu kamili wa kauli katika aya iliyotangulia  na utaelewa umuhimu wa Msimamo katika kutafuta utajiri. Bila ya msimamo  utashindwa hata kabla haujaanza. Kwa msimamo utashinda.

SOMA: Ujumbe muhimu kuhusu kitabu mashuhuri cha Think & Grow Rich.

Ikiwa umewahi kupatwa na jinamizi, utatambua umuhimu wa uvumilivu, umelala kitandani nusu ukiwa macho na mawazo kwamba unakaribia kusongwa rohoni. Unashindwa kugeuka au kusogeza msuli. Unatambua kwamba ni lazima urudishe uthibiti wa misuli yako. Kupitia juhudi za msimamo wa utashi, mwishowe unafanikiwa kusogeza vidole, unaongeza uthibiti wako kwenye misuli ya mkono mmoja, mpaka unaweza kuunyanyua .

Kisha unaongeza uthibiti wa misuli ya mguu mmoja, na kisha unaongeza kwa mguu mwingine. KISHA KWA NGUVU MOJA KUBWA YA UTASHI- unarudisha uthibiti wote juu ya mfumo wako wa misuli na kujinasua kutokana na jinamizi lako. Mbinu hiyo imetendeka hatua kwa hatua.

Unaweza kukuta ni muhimu kujitoa nje ya utepetevu wako wa akili kwa kupitia njia inayofanafana na hiyo, kusogea taratibu mwanzoni, kisha unaongeza kasi yako mpaka unapata uthibiti kamili juu ya utashi wako. Kuwa na msimamo pasipo kujali ni taratibu kiasi gani mwanzoni unaweza kusogea. KWA MSIMAMO HATIMAYE MAFANIKIO YATAKUJA.

Ikiwa utachagua kundi lako la kushauriana kwa umakini, ndani yake utakuwa na angalao mtu mmoja ambaye atakuongoza katika kukuza msimamo. Baadhi ya watu ambao wamepata utajiri mkubwa walifanya hivyo kutokana na mahitaji. Walikuza tabia ya kuwa na msimamo kwa sababu walikuwa na mazingira yaliyowalazimisha kuwa hivyo.

HAKUNA MBADALA WA MSIMAMO! Huwezi mahali pake pakachukuliwa na sifa nyingine yeyote ile! Kumbuka hili mwanzoni na litakupa moyo wakati mambo yatakavyoweza kuonekana magumu na taratibu. Wale waliojitengenezea tabia ya msimamo huonekana kufurahia kinga dhidi ya maanguko. Bila ya kujali ni mara ngapi wameshindwa, mwishowe hufika juu karibu na kileleni mwa mnara. Wakati mwingine huonekana kama kuna muongozaji aliyejificha ambaye kazi yake ni kujaribu watu kupitia aina zote za mazingira yanayokatisha tamaa.

Wale ambao husimama wenyewe baada ya kushindwa na kuendelea kujaribu, hufika na dunia hupiga kelele , “HONGERA NILIJUA UNGEWEZA!” Muongozaji aliyejificha hamruhusu mtu kufurahia mafanikio makubwa bila ya kupitia mtihani wa msimamo. Wale wasioweza kuchukulia rahisi hawawezi kufaulu.

Wale wanaoweza huzawadiwa ukarimu kutokana na msimamo wao. Hupokea kama malipo yao lengo lolote wanalotaka kufikia. Siyo hivyo tu! hupokea kitu fulani kisichopimika muhimu zaidi kuliko malipo ya kitu kinachoshikika-maarifa ambayo KILA ANGUKO HUJA IKIWA NA MBEGU YA FAIDA INAYOLINGANA NALO.

Watu wachache hufahamu kutokana na uzoefu uzuri wa msimamo. Ni wale ambao hawajakubali kushindwa kama kuwa ni kitu chochote zaidi ya kitu cha muda mfupi. Ndio ambao huweka juhudi zao kwa msimamo kiasi kwamba anguko lile mwishowe hugeuka kuwa ushindi. Sisi ambao tunasimama upande wa pili wa maisha huona idadi kubwa sana ya watu wanaoanguka chini katika mapambano pasipo kamwe kuinuka tena.

Tunaona wachache wanaochukua adhabu ya kushindwa kama sababu ya juhudi kubwa zaidi. Hawa kwa bahati hujifunza kamwe kutokukubali gia ya kurudi nyuma ya maisha. Lakini kile tusichokiona, kile ambacho wengi wetu kamwe tusichodhamiria kuwepo ni nguvu iliyo kimya  lakini isiyoshindika ambayo huja kuwaokoa wale wanaoendelea kupambana katika uso wa kukata tamaa.

 UKIPENDA KUSOMA SURA NA SEHEMU ZILIZOPITA BONYEZA HAPA



0 Response to "UFAHAMU WA PESA NI LAZIMA UJENGWE KWA KUTAKA ISIPOKUWA LABDA MTU AZALIWE NAO "

Post a Comment