Ikiwa tutazungumzia
juu ya hii nguvu kwa vyovyoite vile tutaiita msimamo na kuiacha iitwe hivyo.
Kitu kimoja tunachokijua sote, ikiwa mtu hana msimamo hawezi kufikia mafanikio
ya maana katika nyanja yeyote ile.
Mfano mzuri wa nguvu
ya msimamo ni biashara ya burudani. Kutoka duniani kote watu hufika Hollywood
kusaka umaarufu,utajiri, nguvu, mapenzi au chochote kile ambacho binadamu huita
mafanikio. Mara mtu angalipo bado katika kilele cha mafanikio hutoka nje ya
mchakato mrefu wa wasakaji na dunia husikia kwamba mtu mwingine tena amevuna
Hollywood.
Lakini Hollywood
haiwezi kuingilika kirahisi wala haraka. Inakubali vipaji, kutambua uwezo na
hutoa malipo katika fedha tu baada ya mtu kuwa amekataa kukata tamaa na kuacha.
Siri hii kila mara huambatanishwa na neno moja, msimamo! Msimamo ni hali ya
akili hivyo inaweza ikakuzwa kama hali vyingine zote za akili, msimamo unajegwa
juu ya vyanzo halisi vikiwemo;
1. UKAMILIFU WA
LENGO. Kufahamu kile unachotaka ni hatua ya kwanza na pengine muhimu zaidi
kuelekea ujenzi wa msimamo. Sababu yenye nguvu hukulazimisha kushinda vikwazo
vingi.
2. SHAUKU. Ni rahisi zaidi kushika na kudumisha
msimamo katika kufikia lengo la shauku kubwa.
3. KUJITEGEMEA. Imani
katika uwezo wako wa kutekeleza mpango hukupa ujasiri wa kufuata mpango kwa
msimamo(kujitegemea kunaweza kukakuzwa kwa kupitia kanuni zilizoelezwa katika
sura ya 4 juu ya kujishauribinafsi )
4. UKAMILIFU WA
MIPANGO. Mipango iliyopangwa ingawa inaweza ikawa dhaifu isiyotekelezeka kabisa, huchochea msimamo.
5. MAARIFA SAHIHI.
Ukijua kwamba mipango yako ni mizuri kutokana na uzoefu au ushuhuda huchochea
msimamo, kubashiri badala ya kufahamu huua msimamo.
6. USHIRIKIANO.
Huruma, uelewa na ushirikiano muafaka na wengine husababisha kujengeka kwa
msimamo.
7. UTASHI. Tabia ya
kuelekeza sehemu moja fikra zako juu ya ujenzi wa mipango kwa ajili ya
utekelezaji wa lengo kamili husababisha msimamo.
8. TABIA. Msimamo ni
matokeo ya moja kwa moja ya tabia, akili hunyonya na kuwa sehemu ya mazoea ya
kila siku ambayo inajilisha woga, adui mbaya kuliko maadui wote. Waweza
kutibika kikamilifu kwa kurudiarudia kwa nguvu matendo ya ujasiri. Kila mtu
aliyewahi kuona shughuli zinafanyika vitani analifahamu hili.
Kabla ya kuliacha
somo la msimamo, jichunguze mwenyewe tambua ni katika eneo lipi ikiwa lipo una
mapungufu katika sifa hii muhimu. Jipime mwenyewe kwa ujasiri hatua kwa hatua
na uone ni vingapi kati ya vyanzo vya msimamo unavyokosa. Uchunguzi unaweza
kusababisha utambuzi mpya juu yako mwenyewe.
0 Response to "WATU HUMIMINIKA HOLLYWOOD KUSAKA UMAARUFU UTAJIRI NGUVU NA MAPENZI(MAFANIKIO)"
Post a Comment