MICHANGANUO

MICHANGANUO

Duka la Rejareja

Msuya Shopping Centre

1.MUHTASARI TENDAJI.
Utangulizi:
Msuya Shop ni duka la rejareja litakalofunguliwa ndani ya kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo. Lengo la kufungua duka hili ni kutoa huduma bora ya uuzaji wa bidhaa za rejareja kwa wasafiri pamoja na watu wengine wafanyao shughuli zao katika kituo hiki, vilevile ni kuingizia familia kipato zaidi.

Biashara:
Duka hili linamilikiwa kwa ubia na watu wawili, Bwana Joseph Msuya pamoja na Mkewe. Madhumuni makubwa ya kufungua duka hili ni kuboresha zaidi vipato vyao badala ya kutegemea shughuli na bishara walizokuwa nazo awali, kwa mfano duka la bwana Msuya alilokuwa amefungua huko Tandale, mapato yake yalikuwa kidogo kutokana na eneo lenyewe kutokuwa na mzunguko mkubwa wa watu.

Bidhaa:
Watauza bidhaa za aina mbalimbali kama vile unga, nafaka, vyakula vya makopo, vifaa vya usafi majumbani, vifaa muhimu vya wanafunzi mashuleni, vocha za simu na hata vitu vidogo vidogo kama pipi, sindano, uzi na madawa baridi kama asprini na panadol. Ili kufanya muenekano wa duka upendeze na kuvutia makundi ya bidhaa yatapangwa kwa ustadi mkubwa.

Soko:
Soko la bidhaa za rejareja nchini Tanzania hasa katika jiji la Dar es Salaam ni kubwa na limekuwa kimbilio la watu wengi wa tabaka la chini na la kati. Ingawa yapo maduka makubwa (super markets) lakini bado idadi yake ni ndogo sana ukilinganisha na maduka madogomadogo kama Msuya Shop.

Mikakati na Utekelezaji:
Upekee wa Msuya Shop ni eneo duka litakapokuwa. Litafunguliwa ndani ya kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo karibuni na mlango mkubwa wa kutokea watu na magari. Mkakati wao wa masoko utalenga zaidi katika huduma nzuri kwa wateja pamoja na uwekaji bango kubwa juu ya duka litakalokuwa na maandishi juu “MSUYA SHOPPING CENTRE”.

Fedha.
Mauzo ya Msuya Shop kwa mwaka yataongezeka kutoka sh. 65,000,000/=, mwaka 2008 mpaka kufikia sh. 83,720,000/=, mwaka  2010. Kwa upande wa faida yenyewe, haitaongezeka bali kupungua kutoka, sh.7,511,000/= mwaka 2008, sh. 5,096,000/= mwaka 2009 mpaka sh.5,174,000/= mwaka 2010. Hii inatokana na sababu kwamba, katika mwaka wa kwanza gharama za matumizi hasa mishahara zitakuwa chini sana, na huu ni mkakati maalumu wa kuwezesha mtaji ukue kwa haraka.

Faida na hasara Kwa ufupi.



1.1     Dhamira kuu.
Dhamira kuu ya Msuya Shop ni kutoa huduma bora ya uuzaji wa bidhaa za rejareja kwa wasafiri na watu mbalimbali katika kituo kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo, watahakikisha kwamba, wateja wao wanapata bidhaa zote muhimu na kwa haraka ukizingatia kwamba wengi wanakuwa na haraka ya kuwahi kule waendako.

1.2     Malengo:
·        Kuanza kupata faida tangu mwezi wa kwanza na kuendelea.
·        Kuanza kujilipa mishahara  wamiliki kila mmoja sh. 250,000/= ifikapo mwaka 2014.
·        Kufikisha mauzo ya shilingi milioni 80 ifikapo mwaka 2015.

1.3     Siri za mafanikio:
Ili kuweze kuhimili ushindani na kuendelea mbele, Msuya Shop watazingatia mambo matatu yafuatayo kwa umakini.

·        Kuhakikisha mandhari ya duka kwa ujumla inakuwa yakuvutia kwa kufanya usafi na kupanga bidhaa katika mpangilio mzuri.
·     Kubana matumizi kwa kukwepa gharama zisizokuwa za lazima ikiwa ni pamoja na wamiliki wenyewe kutokujilipa mishahara mwaka mzima wa 2013.
·       Kuhakikisha bidhaa zote muhimu na zinazotoka haraka haraka zinakuwepo dukani japo kila aina kidogo kidogo hata kama jambo hili litawalazimu kufanya manunuzi kila mara hasa kipindi ambacho mtaji bado upo chini.

2.Maelezo kuhusu Biashara.
Msuya shop ni duka litakalomilikiwa na Bwana Joseph Msuya pamoja na mke wake Bi, Anastazia Msuya.


Duka hili litafunguliwa ndani ya eneo la kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo, eneo ambalo linasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu mbalimbali wanaotaka kusafiri pamoja na wale wanaorudi kutoka maeneo mbalimbali nje na ndani ya jiji la Dar es salaam.

2.1 Umiliki wa Biashara.
Msuya Shop litasajiliwa kwa msajili wa makampuni kama biashara ya ubia kati ya Bwana Joseph Msuya na Bi Anastazia.Wote wawili watachangia kiasi kilichokuwa sawa cha mtaji, kila mmoja akitoa Sh.900,000/=  jumla zitakuwa Tsh.1,800,000/=.Wanatarajia pia kuchukua mkopo kutoka taasisi isiyokuwa ya kiserikali iitwayo JIENDELEZE Tawi la Ubungo kiasi cha Sh.2,000,000/= ambazo watazirejesha kwa muda wa mwaka mmoja. Mkopo huo utadhaminiwa na samani zao za ndani yakiwemo masofa, kitanda, friji nk. Pamoja na  duka lao jingine lililoko Tandale.

Friji tatu zitahitajika, mbili kati ya hizo zitaazimwa kutoka makampuni ya soda ya Coca cola na Pepsi, lingine watachukua freezer lao kubwa ambalo huwa wanalitumia nyumbani na watalitumia mpaka pale biashara itakapokuwa kiasi cha kununua friji jingine.

Duka la Msuya litafunguliwa ndani ya kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani karibu na lango kuu la kutokea watu, eneo hili lina mzunguko mkubwa wa watu mbalimbali wanaosubiri mabasi na wale wanaoshuka kutoka katika mabasi yanayotokea maeneo mbalimbali nje na ndani ya jiji la Dar es salaam. Fremu ya duka ni kubwa, itakayotosha kupanga bidhaa mbalimbali pamoja  kuweka mafriji matatu.


2.2 Mtaji wa kuanzia.
Gharama za kuanzia pamoja na mtaji wa kuendeshea biashara yenyewe vitatolewa na wamiliki wa biashara hii pamoja na mkopo kutoka shirika la JIENDELEZE(Siyo jina halisi).Vifaa vingine kama mafriji watachukua kutoka nyumbani pamoja na kuazima kutoka makampuni ya soda ya Cocacola na Pepsi. Gharama za awali ni pamoja na usajili, ufuatiliaji wa leseni, dalali wa chumba, kodi ya pango mwezi mmoja kabla biashara haijaanza pamoja na matengenezo madogomadogo.

Mali za kuanzia ni fedha taslimu, bidhaa za kuanzia, samani, mizani ya kupimia vitu pamoja na mali nyinginezo ndogondogo. Jedwali na chati ifutayo vinaelezea kwa ufupi makisio ya gharama za awali na rasilimali za kuanzishia duka hili.



2.3 Eneo Biashara ilipo.
Msuya shop litafunguliwa ndani ya kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo,  eneo ambalo linasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu mbalimbali wanaotaka kusafiri pamoja na wale wanaorudi kutoka maeneo mbalimbali nje na ndani ya jiji la Dar es salaam. Duka litakuwa karibu kabisa na lango kuu la kuingilia na kutokea watu na magari. Upande wa pili linapakana na eneo wanakopumzikia abiria wanaosubiri usafiri na wale waliotoka safarini wakiwasubiri ndugu na jamaa zao. Chumba ni kikubwa kinachotosha kukaa mafriji matatu pamoja na stoo ya kuhifadhia bidhaa.

3.0 Bidhaa.
Msuya shop litauza bidhaa za aina mbalimbali, zinazohitajika na wateja kama yalivyokuwa maduka mengine ya rejareja kuanzia, vinywaji baridi, unga na nafaka mbalimbali, vyakula vya makopo,vifaa vya usafi majumbani,vifaa muhimu vya wanafunzi mashuleni, vocha za simu za mkononi na hata vitu vingine vidogovidogo kama vile pipi, sindano,nyuzi, na madawa baridi kama asprin  na panadol. 

Ili kufanya muonekano wa duka upendeze na kuvutia, makundi ya bidhaa yaliyotajwa hapo juu yatapangwa kwa ustadi mkubwa, kila kundi likipangwa katika eneo lake, upangaji huu utamfanya mteja mara tu aingiapo dukani asipoteze muda mwingi kupepesa macho kujua bidhaa fulani ilipo, hasa hii ni kwa wale wateja ambao huwa hawapendi kuuliza uliza, wanajisikia huru zaidi wanaposema “nipe kitu fulani”, wakati huo tayari anakuwa ameshakiona.

Mteja anayenunua kinywaji baridi atakuwa na hiyari ya kusimama au kukaa kwenye kiti, itategemea ana haraka kiasi gani.


Wengi huwa wanakunywa wakiwa wamesimama kutokana na haraka ya kuwahi usafiri. Saa za kazi ni kuanzia asubuhi saa 12.000 mpaka usiku saa 3.00.

3.1 Tathmini ya Nguvu, Udhaifu, Fursa na Vikwazo.
Biashara ya duka la rejareja inahitaji uzoefu na umakini wa hali ya juu.Uzoefu wa wamiliki wa Msuya shop pamoja na eneo zuri walilochagua ni moja ya nguvu zitakazoifanya biashara hii kupata mafanikio ya haraka. Hatuwezi pia kuacha kutambua udhaifu wao hasa katika suala la mtaji kuwa kidogo, watahitaji juhudi za ziada kuuongeza. Bila kusahau kikwazo kikubwa ambacho ni kuondolewa kwa stendi kuu ya mabasi ya Ubungo kupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi ifikapo mwaka 2014. Ufuatao ni muhtasari wa vitu vilivyotajwa hapo juu;
NGUVU
Ø  Uzoefu wa muda mrefu wa wamiliki wa biashara hii, Bwana Joseph Msuya na mkewe
Ø  Eneo lenye mzunguko mkubwa wa watu duka litakapowekwa ambapo ni ndani ya kituo kikuu cha mabasi Ubungo karibu na lango la kutokea watu na magari.
Ø  Wafanyakazi wa kutosha.
Ø  Kampeni nzuri ya matangazo.

UDHAIFU
Ø Mtaji kidogo.
Ø Kutokuwa na mazoea ya kutosha na watu na mazingira ya kituo.

FURSA.
Ø  Washindani kidogo na wenye mitaji midogo kushinda wakwao.
Ø  Kuongezeka kwa makampuni yanayotengeneza vinywaji baridi hasa maji na soda za kubeba “teki awei”
Ø  Mamlaka ya kituo kudhibiti biashara ndogondogo hasa wamachinga wanaotembeza bidhaa mikononi kuingia kituoni kiholela.


VIKWAZO.
Ø Kituo kuwekwa katika mpango wa kubadilishwa na kuwa stendi ya mabasi yaendayo kasi ifikapo mwaka 2014.
Ø Kuongezeka kwa maduka makubwa(super markets) hasa nje ya kituo.
Ø Hali ya uchumi  kutotengemaa pamoja na mfumuko wa bei kuendelea kupaa.

4.0  Uchambuzi wa soko.
Sekta ya biashara ya rejareja nchini Tanzania ni sekta kubwa na ambayo imekuwa kimbilio la watu wengi wa tabaka la chini na lile la watu wa kati ingawa yapo pia maduka makubwa machache (super markets) hasa katika jiji la Dar es salaam. Soko watakalolenga zaidi ni abiria wanaosubiri usafiri na wale wanaotoka safarini maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Washindani wakubwa wa Msuya Shop ni maduka yanayopakana nalo, kama vile Hamza Shopping Centre, Upendo Shop na H.K Dissabled Kiosk

4.1 Mgawanyo wa soko.
Msuya shop linategemea kutoa huduma zake kwa jamii yote inayolizunguka eneo lililopo duka pamoja na wateja wanaoingia na kutoka kila siku katika kituo hiki cha Ubungo.Wengi wa watu katika kituo hiki ni wale wanaosubiri usafiri kuelekea maeneo mbalimbali, wanaoshuka kutoka kwenye mabasi yanayotoka sehemu mbalimbali, wanaowasindikiza ndugu na jamaa hao, wanaowasubiri ndugu na jamaa zao watakaokuja na mabasi  kutoka maeneo mbalimbali, kundi jingine la watu ni wale wanaofanya shughuli zao kila siku ndani ya kituo hiki kama vile,wakata tikiti, wafanyibiashara, walinzi, mafundi, askari na wafanyausafi.


4.2 Soko lengwa.
Duka hili pamoja na kutoa huduma zake kwa kila mtu miongoni mwa makundi yote ya watu waliotajwa hapo juu, lakini litalenga zaidi makundi haya mawili; wanaosubiri mabasi na wale wanaoshuka kutoka kwenye mabasi. Makundi haya mbali na  kuwa idadi yao ni kubwa kila siku, pia wanao uwezo mkubwa  wa kufanya manunuzi hasa vinywaji na vitafunwa vinavyobebeka “take aways” kwa fedha ambazo wanakuwa wameshazitenga kabisa maalumu kwa kazi hiyo kabla ya kuanza safari.

Hasa hasa wale wanaoshuka kutoka kwenye mabasi wanakuwa hawana uchaguzi, kwani kutokana na kukaa muda mrefu ndani ya basi wanakuwa wamechoka na kuwa na kiu, hivyo kuhitaji kupumzika kidogo huku wakipooza koo  kabla hawajatafuta usafiri wa kuwafikisha makwao maeneo mbalimbali jijini.



Tathmini ya soko.
2008
2009
2010
Wateja watarajiwa
Ukuaji.
Wanaosubiri mabasi kuelekea mikoani
2%
70,000
71,400
72,828
Wanaoshuka kutoka kwenye mabasi.
2%
40,000
40,800
41,616
Wanaosindikiza au kuwasubiri jamaa zao
2%
25,000
25,500
26,010
Wanaofanya kazi zao kituoni
1%
15,000
15,150
15,302
Jumla.
2%
150,000
152,850
155,756


4.2.1 Muelekeo na mahitaji ya soko.
Soko la bidhaa za rejareja linaendelea kukua siku hadi siku kutokana na ukweli kwamba idadi ya watu katika jiji la Dar es salaam na hususani katika mikusanyiko ya watu kama vituo vya mabasi nayo inaongezeka kwa kasi kubwa.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2002  wilaya ya Kinondoni kilipo kituo cha Ubungo  ilikuwa na watu wapatao milioni 1 na mpaka kufikia mwaka 2008 inakadiriwa idadi hiyo imeongezeka na kufikia watu wapatao milioni 14 katika ongezeko la asilimia 4.1% kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Tovuti ya jiji la Dar es salaam idadi ya  watu wanaoingia na kutoka ndani ya kituo kila siku wanakadiriwa kufikia 30,000. Kituo kina jumla ya Migahawa na baa zaidi ya 25, maduka/vibanda zaidi ya 106  ambavyo vyote hutoa huduma kwa wasafiri na watu mbali kituoni hapo na maeneo jirani.

4.3  Uchambuzi wa sekta.
Sekta ya biashara ya rejareja nchini Tanzania ni sekta kubwa na ambayo imekuwa kimbilio la watu wengi wa tabaka la chini na lile la watu wa kati. Ingawa yapo maduka (super markets) hasa katika jiji la Dar es salaam, lakini bado idadi yake ni ndogo sana jambo linalofanya idadi kubwa ya watu kuendelea kununua bidhaa za rejareja kutoka katika maduka madogomadogo kama Msuya shop.

Maduka ya rejareja hununua bidhaa zake nyingi kutoka katika maduka ya jumla ambayo nayo ni mengi hasa katika maeneo ambayo watu wengi wamefungua maduka ya rejareja.Wengine kwa kutaka kununua kwa bei nafuu hufuata maduka ya jumla yaliyopo katikati ya mji kama vile Kariakoo na Mnazi mmoja lakini ni kwa wale tu waliokuwa na mitaji mikubwa.

Kwa wale ambao mitaji yao bado haijakua kama Msuya shop hulazimika kununua kutoka katika maduka yaliyopo karibu ili kupunguza gharama. Msuya shop katika kipindi hiki linapoanza mtaji ungali bado kidogo  watalazimika kubana matumizi sana na hata ikiwezekana kununua bidhaa kutoka kwa watu wanaosambaza wenyewe mitaani kwa miguu, pikipiki, baiskeli na magari, lakini pia kwa tahadhari kubwa wasije wakauziwa kwa bei kubwa kushinda bei ya soko.

4.3.1 Ushindani.
Washindani  wakubwa wa Msuya shop ni maduka yanayopakana nalo, kama vile Hamza Shopping Centre, Upendo Shop na H.K Dissabled Kiosk.Vile vile wapo wauzaji bidhaa mbalimbali mikononi wanaotembeza maarufu kama wamachinga ingawa hawa siyo wengi kutokana na mamlaka ya kituo kuwazuia, wale wanaoingia hufanya hivyo kwa vibali maalumu wanavyolipia. Mshindani wao mkubwa zaidi ni Hamza Shopping Centre ambalo ni duka kubwa  lenye bidhaa nyingi karibu aina zote wanazotarajia  kuziweka.

Hamza Shopping wanaye mfanyakazi mmoja tu ambaye ndiye huyo huyo anayefanya kazi ya kuuza, vilevile wanae kibarua ambaye hutumwa kufuatilia mizigo maduka ya jumla. Kutokana na kuzidiwa na shughuli nyingi, muuzaji huyo mmoja hulazimika kuchelewa kufungua duka na pia huwahi kufunga mapema saa 12.00 jioni. Hawa washindani wengine waliobakia Upendo na H.K, mitaji yao ni midogo sana ukilinganisha na Msuya shop, huweka bidhaa chache sana hasahasa vinywaji baridi na vitafunwa, ambavyo vingi huwa ni  keki na bagia.

Msuya shop watasahihisha mapungufu yote waliyokuwa nayo washindani wao, kwa kuwa na timu ya watu watatu, watakaofanya kazi kwa kujituma kutokana na kulipwa vizuri.Timu hiyo itakuwa na muuzaji mmoja, Bi anastazia, Meneja atakayehusika pia na ununuzi wa bidhaa, huyu atakua Bwana Joseph Msuya mwenyewe na watatu ni mfanyakazi atakayeajiriwa maalumu kwa ajili ya kazi za kuhudumia wateja nje ya duka.

Watahakikisha pia wanaweka mchanganyiko wa bidhaa mbalimbali kukidhi mahitaji ya wateja wao wote kwa ukamilifu, ikiwa ni pamoja na mpangilio mzuri wa bidhaa na kuweka mazingira yote yanayolizunguka duka katika hali ya usafi kuwavutia wateja.


5.0  Mikakati na Utekelezaji.
Msuya shop litatofautiana na maduka mengine, kutokana na vigezo vikuu viwili, eneo duka litakapokuwa ambapo ni kandokando ya mlango mkuu wa kutokea, pamoja na uzoefu wa muda mrefu wa wamiliki wake katika shughuli za biashara ndogondogo.Mafanikio yatatokana pia na mikakati mizuri ya matangazo ambayo ni uwekaji wa bango kubwa juu ya paa la duka, vipeperushi, huduma nzuri kwa wateja na salamu redioni.

5.1 Sifa za kipekee.
·    Upekee wa Msuya shop ni eneo litakapowekwa duka, eneo hili lipo ndani ya Kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo, karibu na lango kubwa ambalo watu na magari hutokea na kuingia.
·    Sifa nyingine ni uzoefu wa muda mrefu  wa wamiliki wa duka hili katika shughuli za biashara hususani hii ya rejareja.

5.2  Mkakati wa soko.
Mkakati wa soko utalenga zaidi katika huduma nzuri kwa wateja pamoja na mpangilio wa bidhaa unaovutia,vile vile litawekwa bango kubwa juu ya paa la duka lenye maandishi makubwa yanayosomeka “MSUYA SHOPPING CENTRE”

·   Bei: Watatoza bei za kawaida zisizokuwa kubwa sana wala ndogo sana, huku wakiwa makini mno kuhakikisha  bei zao haziwi juu kupita za washindani wao. Pia watahakikisha ya kwamba hawatozi bei za chini kuwavutia wateja ikiwa kwa kufanya hivyo watapata hasara.

· Matangazo:-Kabla ya ufunguzi rasmi watatengeneza vipeperushi kuwajulisha wateja wao kuwa wapo. Bango kubwa lenye jina “MSUYA SHOPPING CENTRE” litawekwa juu ya paa la duka. Wataanzisha pia mpango wa kutuma salamu kwenda kwa watu tofauti katika radio mbalimbali ikiwemo radio maalumu inayotangaza katika kituo huku likitajwatajwa jina la Msuya shop.

5.3 Mkakati wa mauzo.
Muuzaji atatabasamu na wateja kila mara waingiapo pamoja na kuwa na lugha nzuri huku akizingatia kuwa, “mteja hakosei”.Hii itawafanya wateja waendelee kununua dukani mara kwa mara huku wakieneza na kwa watu wengine sifa nzuri za Msuya Shop.

5.3.1 Makisio ya mauzo.
Makisio ya mauzo miezi ya mwanzo yatakuwa madogo, lakini baada ya wateja kuzoea mauzo yataanza kupanda. Vilevile miezi ya likizo kama June, July, November na Disemba mauzo yatakuwa juu zaidi kutokana na watu kuwa wengi kituoni hasa wanafunzi na wafanyikazi serikalini na makampuni wanaosafiri kwenda mikoani. Mauzo kwa siku yanaonekana kuwa makubwa lakini faida kidogo kutokana na bidhaa nyingi hasa vocha za simu kuwa na mauzo makubwa lakini faida kidogo.






































Makisio  ya mauzo.

2008
2009
2010
Mauzo.
               Sh.
Sh.
Sh.
Mauzo yote.
65,000,000
72,800,000
83,720,000
Mengineyo.
0
0
0
Jumla ya Mauzo yote.
65,000,000
72,800,000
83,720,000





2008
2009
2010
Gharama za mauzo.
45,500,000
50,960,000
58,604000
Nyinginezo.
0
0
0
Jumla gharama za mauzo.
45,500,000
50,960,000
58,604000

5.4  Utekelezaji wa matukio muhimu.

Ili kuhakikisha mambo yanakwenda kama yalivyopangwa katika maandalizi ya ufunguzi wa Msuya Shop, jedwali lifuatalo linaorodhesha matukio muhimu yatakayotekelezwa, pamoja na tarehe bajeti na mtu atakayehusika.


Matukio muhimu.
Vitendo.
Tarehe ya kuanza
Tarehe ya kumalizia.
Bajeti Tsh.
Mhusika
/Meneja
Idara
Kutengeneza mchanganuo wa biashara
1/8/2007
5/9/2007
60,000
Joseph. M
Utawala
Kuangalia eneo.
15/8/2007
15/8/2007
0
Joseph. M
Utawala
Ukarabati.
1/9/2007
15/9/2007
30,000
Joseph. M
Utawala
Leseni.
1/10/2007
2/10/2007
1,000
Anastazia.M
Utawala
Maswala ya mkopo.
15/10/2007
1/11/2007
0
Anastazia.M
Utawala
Kuweka bango.
1/1/2008
1/1/2008
50,000
Joseph. M
Utawala
Ufunguzi.
2/1/2008
3/1/2008
0
Anastazia.M
Utawala
Jumla.
141,000
                                                                                

6.0 Maelezo kuhusu Utawala.
Kama tulivyokwishasema mwanzoni, Msuya Shop itakuwa biashara ya ubia kati ya Bwana Joseph Msuya na mkewe Bibi Anastazia Msuya. Bibi Anastazia ndiye atakayekuwa mwuzaji na Bwana Joseph yeye atakuwa meneja,watamuajiri mtu mwingine mmoja ambaye majukumu yake yatakuwa ni kuhudumia wateja nje pamoja na shughuli nyingine ndogondogo zitakazojitokeza kama vile ubebaji wa bidhaa kuingiza ndani pamoja na kumsaidia Bibi Anastazia kazi za usafi.

Bwana Joseph Msuya baada ya kumaliza elimu yake ya msingi huko Mkoani Kilimanjaro mwaka 1990, alikuja jijini Dar es salaam na kuajiriwa na kaka yake kama muuzaji wa duka la rejareja pale Kariakoo. Baada ya miaka sita kaka yake alimpa mtaji, akaenda kufungua duka lake mwenyewe la rejareja huko Tandale kwa Tumbo ambalo analo mpaka sasa hivi. Kwa sasa ameamua yeye na mkewe wafungue duka jingine Ubungo Stendi kuu watakaloliita  Msuya shopping centre.

Bibi Anastazia yeye ana cheti (Advanced certificate) kutoka chuo cha Biashara CBE jijini Dar es salaam katika maswala ya masoko alichotunukiwa mwaka 2000.

Amewahi kufanya kazi katika makampuni mbalimbali yakiwemo Coca cola, Pepsi,na Azam kama mtu wa masoko na hata amewahi kuwa afisa masoko wa kanda ya ilala katika kampuni ya maji ya kunywa ya Masafi.Mwaka huu ameamua kuachana na kazi za kuajiriwa na kuunganisha nguvu na mumewe waanzishe Msuya shop. 

6.1  Mpango wa malipo.
Wakati duka linapoanza katika mwaka wa kwanza, litakuwa na mtaji kidogo, hivyo itabidi kufanya kila linalowezekana kubana matumizi ili mtaji uongezeke haraka haraka.Mbinu watakayoitumia ni pamoja na wamiliki wenyewe kutokujilipa mishahara katika mwaka mzima wa 2009, lakini mfanyakazi watakayemwajiri atalipwa kama kawaida na ataanza na mshahara wa Sh. 150,000/= mwaka wa pili na wa tatu Msuya na Mkewe wataanza kujilipa mishahara kama kawaida kwani mtiririko wa fedha utakuwa umekwishaanza kuwa mzuri.


Mpango wa mishahara.

2008
2009
2010

Sh.
Sh.
Sh.
Bwana Joseph  Msuya.
0
2400,000
3,000,000
Bibi  Anastazia  Msuya.
0
2400,000
3,000,000
Mtoa huduma.
1,800,000
2400,000
2400,000
Jumla ya watu.
3
3
3
Jumla ya mishahara.
1,800,000
7,200,000
8,400,000

7.0 Mpango wa Fedha.
Yafuatayo ni makisio ya fedha kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo. Fedha kwa ajili ya  mahitaji ya kuanzia zitatokana na mtaji wa wamiliki  wenyewe  jumla ya Sh.1,800,000/=  pamoja na mkopo wa muda mfupi kutoka shirika la JIENDELEZE sh.2,000,000/=
Jumla zote kwa pamoja ni sh.3,800,000/= Kiasi hiki cha fedha japo kitatosha kuanzia lakini bado ni kidogo kuweza kununua bidhaa zote kwa kiwango cha kutosha.

Miezi ya mwanzoni mwa mwaka 2008 watanunua ‘stock’ kidogo kidogo ya bidhaa ili angalao waweze kununua kila bidhaa iliyokuwa muhimu na zile ambazo utokaji wake ni wa haraka haraka tu. Matokeo ya kubana matumizi pamoja na ununuaji wa bidhaa chache lakini kila mara tena zile zenye mzunguko mkubwa yatasababisha mtaji uweze kuongezeka haraka hivyo mtiririko wa fedha taslimu kuimarika na hatimaye kila bidhaa zianze kununuliwa kwa wingi na katika ‘stoku’ inayotosheleza kwa kipindi kirefu.


7.1 Makisio muhimu.
§  Wanakisia ukuaji mzuri wa soko usiokuwa na vizuizi vingi.
§  Hawategemei kuuza kwa mkopo, labda kama itatokea itakuwa ni kwa mara chache sana tena kwa tahadhari ya hali ya juu.
§  Riba ya mkopo kwa mwaka inakadiria kiwango cha wastani wa asilimia 28% kulingana na viwango vya miaka iliyopita.

§  Kodi ya mapato kwa mwaka inakadiriwa wastani wa asilimia 30% ya faida kabla ya riba na kodi kwa mwaka.

7.2 Tathmini ya kiasi cha mauzo yanayohitajika kurudisha gharama zote zitakazotumika kwa mwezi.


Ili waweze kurudisha gharama  zote kwa mwezi itabidi  kiasi cha mauzo kisipungue shilingi.1,573,332, jedwali na chati vifuatavyo vinafafanua zaidi.



















Tathmini ya kiasi cha mauzo.

Kiasi cha mauzo yatakayorudisha gharama kwa mwezi.
Sh.1,573,332
Makisio.

Wastani wa asilimia ya gharama zinazobadilika (%)
75%
Gharama za kudumu kwa mwezi.
Sh.393,333









7.3  Makisio ya ripoti ya faida na hasara.

·    Majedwali yafuatayo yanaonyesha  makisio ya faida na hasara kwa kila mwezi  katika mwaka wa kwanza na kisha kwa kila mwaka katika miaka mitatu inayofuata.










































































MAKISIO YA RIPOTI YA FAIDA NA HASARA

2008
2009
2010

Sh.
Sh.
Sh.
MAUZO.
65,000,000
72,800,000
83,720,000
Gharama za mauzo .
48,750,000
54,600,000
62,790,000
Faida Ghafi.
16,250,000
18,200,000
20,930,000
%Faida ghafi kwa mauzo.
25%
25%
25%

Gharama za uendeshaji.



Mishahara.
1,800,000
7,200,000
8,400,000
Kodi ya pango.
2,400,000
3,000,000
3,000,000
Umeme.
360,000
420,000
420,000
Ushuru wa taka.
60,000
100,000
100,000
Mengineyo.
100,000
200,000
200,000
Jumla ya gharama za uendeshaji.
4,720,000
10,920,000
12,120,000
Faida kabla ya kodi na riba.
11,530,000
7,280,000
8,810,000
Riba ya mkopo.
560,000
0
0
Kodi ya mapato 30%
3,459,000
2,184,000
3,636,000
Faida halisi.
7,511,000
5,096,000
5,174,000
%Faida halisi / mauzo.
11.5%
7%
6%



















7.4 Makisio ya Ripoti ya  Mtiririko wa Fedha.

Ifuatayo ni chati na jedwali la makisio ya mtiririko wa fedha.


















MAKISIO YA RIPOTI YA MTIRIRIKO WA FEDHA.

2008
2009
2010
FEDHA ZINAZOINGIA.
Sh.
Sh.
Sh.
Kianzio
2,000,000
6,960,996
10,356,996




Mauzo Taslimu
65,000,000
72,800,000
83,720,000
Makusanyo ya deni toka kwa wateja.
0
0
0
Mkopo mpya wa muda mfupi.
0
0
0
Mkopo mpya wa muda mrefu
0
0
0
Uuzaji wa mali za kudumu.
0
0
0
Mtaji mpya.
0
0
0
JUMLA YA FEDHA INGIA.
65,000,000
72,800,000
83,720,000

FEDHA ZINAZOTOKA.



Ununuzi wa bidhaa kwa fedha taslimu.
49,300,000
54,150,000
67,960,000
Ulipaji wa fedha taslimu.
4,719,996
10,920,000
12,120,000
Ulipaji wa bili mbalimbali(madeni ya wateja)
0
0
0
Urejeshaji mkopo  wa muda mfupi.
2,000,000
0
0
Urejeshaji mkopo  wa muda mrefu.
0
0
0
Ulipaji riba ya mkopo.
560,000
0
0
Ulipaji wa kodi ya mapato.
3,459,000
2,184,000
3,636,000
Ununuzi wa mali za muda mfupi.
0
0
0
Ununuzi wa mali za kudumu.
0
0
0
Utoaji wa gawio.
0
0
0
JUMLA YA FEDHA ZOTE ZINAZOTOKA.
60,038,996
67,254,000
83,716,000
Mtiririko wa fedha.
4,960,996
5,546,000
4,000
SALIO LA MWISHO.
6,960,996
10,506,996
10,510,996


























7.5  Makisio ya Ripoti ya  Mali na Madeni.

MALI  NA  MADENI.
2008
2009
2010
Sh.
Sh.
Sh.


MALI


Mali za muda mfupi


Fedha taslimu
6,960,996
10,356,996
10,356,996
Wadaiwa/wateja
0
0
0
Bidhaa za stoo
1,550,000
3,250,000
8,424,004
Mali nyinginezo za mda mfupi
0
0

Jumla ya mali za muda mfupi.
8,510,996
13,606,996
18,781,000

Mali za kudumu
200,000
200,000
200,000
Uchakavu
0
0
0
Jumla mali za kudumu.
200,000
200,000
200, 000
JUMLA MALI ZOTE
8,711,100
13,806,996
18,981,000

MADENI NA MTAJI


Wadai/wateja
0
0
0
Deni la mda mfupi/taasisi
0
0
0
Deni la mda mrefu/benki
0
0
0
Jumla ya deni lote
0
0
0

MTAJI wa mmiliki.
1,800,000
1,800,000

1,800,000
Faida iliyolimbikizwa.
(600,000)
6,911,000
12,007,000
Faida.
7,511,100
5,096,000
5,174,000
Jumla ya mtaji
8,711,100
13,807,000
18,981,000

JUMLA YA MTAJI NA DENI
8,711,100
13,807,000
18,981,000


7.6 Sehemu muhimu.


2008
2009
2010
Ukuaji wa mauzo.
0%
12%
15%

Asilimia ya mauzo.



Mauzo.
100%
100%
100%
Faidaghafi.
25%
25%
25%
Jumla ya gharama za uendeshaji.
7%
15%
14%
Faida halisi
12%
7%
6%

Asilimia ya Mali zote.



Mauzo kwa mali zote
746%
527%
441%
Wadaiwa.
-
-
-
Mali za muda mfupi
13%
19%
22%
Mali za kudumu.
0.30%
0.27%
0.24%
Deni
-
-
-
Jumla ya mtaji
13%
19%
23%

Sehemu nyinginezo.



Bidhaa za stoo kwa jumla ya mali.
0.17
0.24
0.44
Uwiano sasa (current ratio)
-
-
-
Uwiano haraka (Quick ratio)
-
-
-
Jumla ya mali kwa mauzo yote.
0.13
0.19
0.23



















MCHANGANUO HUU BADO HAUJAISHA UTAENDELEA.....................

26 Responses to "MICHANGANUO"

  1. Nahisi sijachelewa sana kuifahamu hii blog, nimejikuta tu naipenda ghafla kutokanana maarifa yaliyomo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli kabisa Prosper, wala hujachelewa kabisa kwani safari nzima ya binadamu hapa duniani imezungukwa na biashara kwa kiasi kikubwa hivyo ujasiriamali upo na utaendelea kuwepo muda wote wa uhai wetu.

      Delete
  2. Replies
    1. Thank you very much Mr/Miss Unknown for your appreciation!

      Delete
  3. Vizuri sana,nimependa blog yenu, ninauhitaji wa andiko la mradi wa kilimo cha kitunguu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana Daniel, sisi kwa sasa tunashughulika na uelimishaji kupitia vitabu na blogu tu peke yake, hatujaanzisha huduma ya kuandika michanganuo specific kwa ajili ya mtu mmojammoja.

      Delete
    2. This comment has been removed by a blog administrator.

      Delete
  4. Hakika unastahili pongezi. Najuta kwa nini sikukufahamu mapema. Mimi ndo nipo kwenye hata za uendeshaji kiwanda kidogo. Naamini maarifa yako yataniwezesha kuvuka pale nilipokuwa na utata. Ubarikiwe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana Mr. Kyamani, na mwaka huu wa 2019 viwanda ndiyo kauli mbiu yetu kubwa hivyo tutakuwa na michanganuo mingi inayohusiana na viwanda vidogo na vya kati.

      Delete
    2. Mr. Peter Augustine nimefurahi sana kupata ukurasa huu. Sijui namna ntakavyosoma Tena majibu Yako baada ya kutoka Sasa. Nawezaje kuingia kwenye blog ili niendelee kujifunza

      Delete
    3. Nakushukuru sana kutoa hii Elimu. NAMI nataka kuanzisha Biashara na nilihitaji sana kufahamu kuandika mchanganuo wa Biashara. Asante sana najifu za sasa

      Delete
  5. Hii blog inafundisha sana nadhani kwangu Mimi nimejifunza kitu ahsante sana ubarikiwe

    ReplyDelete
  6. So nice guys, I appreciate your work. Naweza kuwa napata post zenu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mr. Ferus we appreciate too, post zetu tunapoweka hapa katika hii blog unazipata lakini pia unaweza kusubscribe hapo katika JIUNGE NA BLOG YETU utapata makala mbalimbali ambazo wakati mwingine hatuziweki hapa bloguni. ASANTE SANA!

      Delete
  7. Sehemu sahihi katika kutimiza malengo yangu ni hapa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante, tupo pamoja na tutaendelea kuwa pamoja sana!

      Delete
  8. Ahsante sana kwa elimu nzuri hakika umenifungua macho na akili pia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana na wewe ndugu Mbuya kwa kusoma hapa

      Delete
  9. Hii kitu ni tamu Sana... nashukuru Sana Kwa mchanganuo Kwa kweli ukiuheshimu huu mpango ktk business yako HAICHOMOKI

    ReplyDelete
  10. naaam nashukuru sana Umefungua ubongo wango wangu kwa % nyingi sana
    MUNGU AKUBARIKI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Immatailor Mungu akubariki na wewe pia, tupo pamoja mkuu!

      Delete
  11. Asante sana kwa kazi nzuri. Nahitaji kupata mpango biashara na kupata nondo zinazotolewa. Nahisi nimechelewa nisaidie niinuke ndugu yangu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unakarinishwa sana ndugu yangu tuwasiiane tu michangauo ipo na nondo za kumwaga

      Delete