Pinda: changamkieni fursa zilizopo. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

Pinda: changamkieni fursa zilizopo.

Ludewa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameawataka wananchi wilayani Ludewa kuchangamkia fursa katika miradi, ili wanufaike kwanza kabla ya watu kutoka nje.
Waziri mkuu Mizengo Pinda.

Akihutubia mkutano wa hadhara viwanja vya mpira wa miguu Ludewa juzi, Pinda alisema miradi ya mkaa wa mawe na chuma, ni hatua nzuri.

Pinda alisema tayari wawekezaji wapo hatua za mwisho ifikapo mwaka 2014,miradi hiyo itaanza hatua za uzalishaji wa chuma na umeme.

Kufuatia kuanza kwa miradi hiyo, Pinda aliagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuandaa wananchi kwa kutoa elimu kuhusu fursa. Megawati 600 za umeme zinatarajiwa kuzalishwa.

“Bila maandalizi mazuri kwa wananchi wa Ludewa, kuna hatari ya kugeuka watazamaji katika mali waliyolinda kwa zaidi ya miaka 50,” alisema Pinda.
Alisema kazi ya Serikali hivi sasa ni kuhakikisha inajenga barabara kupitisha mitambo inayotakiwa kwenye miradi hiyo na kwamba, tayari Sh7 bilioni za awali zimetengwa kwa upanuzi wa barabara.

Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kutoka Itoni, Ludewa hadi Manda, Waziri Pinda alisema tayari Serikali imetenga fedha za upembuzi yakinifu, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi.
Akizungumzia sekta ya kilimo, Pinda alisema jembe la mkono haliwezi kumaliza matatizo ya mkulima, kinachotakiwa ni kuangalia uwezekano wa kuwakopesha wakulima matrekta ya bei nafuu

0 Response to "Pinda: changamkieni fursa zilizopo."

Post a Comment