Wizara ya Kazi na Ajira kwa kushirikiana na Benki ya CRDB
imezindua mpango wa kukuza ajira kwa vijana 30,000 kwa kuwapatia mikopo
wahitimu wa vyuo vikuu vya elimu ya juu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki
hii, Msemaji wa wizara hiyo Ridhiwani Wema, alisema lengo la mpango huo ni
kuongeza idadi ya vijana wanaomiliki shughuli rasmi za kiuchumi na waweze
kujiajiri na kuajiri wengine na kukuza utamaduni wa kijasiriamali pamoja na
ubunifu.
“Serikali imeamua kutoa fursa kwa vijana 30,000 za moja kwa moja
kwa wahitimu wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitatu na kuwawezesha wenzao
wa kada ya uchumi wasiopungua 100,000, ajira hizi zitakuwa ni za moja kwa moja
mbali na zile zitakazotokana na mnyororo mzima wa thamani” alisema Wema.
Alisema serikali imekubaliana na benki ya CRDB kuanzisha utoaji
wa mikopo kwa vijana mara utekelezaji wa program utakapoanza.
Pia alisema kuwa mpango huo utatekelezwa na serikali kwa
kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu nchini, taasisi za fedha na wabia wa
maendeleo.
CHANZO: NIPASHE
0 Response to "Wahitimu wa vyuo vikuu kuwezeshwa mikopo kujiajiri"
Post a Comment