Ni tangu kuzaliwa
Hawajawahi kuonana na binadamu.....
Watoto watatu huko Accra nchini Ghana, wasichana wadogo
wawili na watatu mkubwa, mvulana wa miaka 8 wamekuwa wakishirikiana chumba
kimoja na mifugo, bata, kuku na kondoo huku wakiwa hawajawahi hata siku moja
kuonana na binadamu wengine wowote zaidi ya wazazi wao tangu walipozaliwa.
Mwandishi, Beatrice Adu wa mtandao wa Joys News, aliyekuwepo
katika eneo la nyumba walimokutwa watoto hao katika mji wa Madina alisema,
watoto hao watatu walikuwa wakiishi katika mazingira machafu kupindukia.
Alisema sehemu ya nyuma ya nyumba inayoelekea vyumba vinne vya kulala
kulikuwa na zizi la mifugo lililojaa mabata mizinga, kuku, na kondoo. Maeneo
kuzunguka nyumba yalijaa magugu, Beatrice alisema. Akaongeza kwamba na korido
inayoelekea chumba cha watoto hao ilijaa harufu mbaya na uvundo mzito.
Wakizungumza na Beatrice watoto hao walimuambia kwamba,
wazazi wao walikuwa wakiwaambia kwamba kila mtu nje ya nyumba yao alikuwa
mbaya. Mama wa watoto hao, Jane Mensah, alisema watoto hawaendi shuleni kwasababu
baba yao Fledge Mensah Lartey anaweza kuwafundisha mwenyewe nyumbani.
Kamanda wa Polisi wa Madina aliuambia mtandao wa Joy News
kwamba, ofisi yake ikishirikiana na kitengo cha ustawi wa jamii walikuwa
wanaandaa makazi ya muda kwa watoto hao wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.
Naye Daktari mkuu wa magonjwa ya akili Dr.Kwasi Osei alisema
wazazi wa watoto hawa hasa baba yao inawezekana wanasumbuliwa na ugonjwa wa
akili, ‘uwendawazimu’ Ugonjwa ambao unamfanya mtu kuwa na hofu ya
vitu visivyojulikana. “Mtu anayesumbuliwa na ugonjwa huu hufikiria watu wengine
wanaomzunguka wanamuwinda yeye na watoto wake na hivyo kuwazuia wasichanganyike
na watu wengine. Wanaamini watu wengine ni ‘shetani’, watu waovu.
CHANZO: Mtandao wa myjoyonline.com

0 Response to "WATOTO WAFUNGIWA NDANI NA MIFUGO MIAKA 8 BILA KUONA NJE"
Post a Comment