BIASHARA YA FILAMU HAICHAGUI UMRI. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BIASHARA YA FILAMU HAICHAGUI UMRI.



Biashara ya filamu na sanaa kwa ujumla haichagui una umri gani, inaweza kukutoa hata ikiwa upo chini ya miaka 18, kinachotakiwa tu ni kipaji pamoja na juhudi za kutosha. Hebu tazama msanii kama Lulu ambaye amefanya uzinduzi wa filamu yake mpya “FOOLISH AGE” usiku wa jana. Kampuni iliyoamua kumdhamini “Proin Promotion”,  sidhani  kama ilifanya hivyo kwa kuwa Lulu ni mrembo sana,  bali nafikiri imeona fursa ya kutengeneza faida iliyokuwepo kutokana na kipaji na umaarufu aliokuwa nao Lulu. Pamoja na uchanga wake Lulu ameweza kupiga hatua kubwa kiusanii.
Picha ni kwa hisani ya http://www.bongoclantz.com

0 Response to "BIASHARA YA FILAMU HAICHAGUI UMRI."

Post a Comment