HATIMAYE KILIO CHA GWIJI MAALIM GURUMO CHAPATA MAJIBU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HATIMAYE KILIO CHA GWIJI MAALIM GURUMO CHAPATA MAJIBU


Kwa wiki kadha tokea kustaafu kwa  gwiji wa muziki wa dansi nchini Mzee Muhidin Gurumo  huku akilalamika kuwa katika hali ya ukata mkubwa kiasi cha kuhudhuria hospitalini anakotibiwa matatizo ya kiafya kwa kusukumana kwenye daladala na abiria wengine, wadau mbalimbali walipaaza sauti zao wakiwataka Watanzania na watu wote wenye mapenzi mema kutafakari ni kwa namna gani wanaweza wakamuenzi huyu shujaa wetu katika upande wa burudani angali bado duniani. Sasa vilio hivyo vimeanza kuzaa matunda baada ya msanii wa muziki Nasib Abdul au ‘Diamond Platinumz’ kumzawadia gari jana usiku katika uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya uitwao “Number one”  ukumbi wa Serena Hotel  jijini Dar.



Pichani juu ni gari aina ya FunCargo lenye namba za usajili T789 AYS alilopewa Mzee Muhidin Gurumo.



CHANZO: .bossngasa.com/ na GPL

0 Response to "HATIMAYE KILIO CHA GWIJI MAALIM GURUMO CHAPATA MAJIBU"

Post a Comment