Mwenge wa Uhuru licha ya maana yake kuwa nzuri na
yenye faida nyingi katika kuleta umoja wa kitaifa, upendo na amani hasa siku
hizi ambapo vitu hivyo vimeanza kutoweka, lakini wapo watu au makundi ya watu
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiitikadi wamekuwa wakiuponda na
kuonyesha kwamba hauna faida yeyote na hata ungefaa ufutiliwe mbali.
Watu wengine hudai kwamba kila panapokuwa na mikesha
ya mwenge, asubuhi mahali hapo hukutwa mipira kibao ya kiume imetapakaa,
ikiashiria palitendeka vitendo vya kizinzi usiku. Lakini la kujiuliza ni kwamba
vitendo hivyo hufanywa na wanyama au binadamu wenye akili na utashi? .Matendo mabaya ya kizinzi hayachagui
mahali pa kufanyiwa ilimradi tu pamekuwa na giza au usiri, kwani hujawahi kusikia habari za viongozi wa dini kutenda
mambo hayo tena ndani ya nyumba za ibada wanapojua hamna mtu anayemuona?
Hakuna nchi duniani isiyokuwa na tunu zake za
kitaifa, yapo mambo unaweza ukayaona ya kijinga lakini, umuhimu wake utaujua
pale utakapo achana nayo. Wakati Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Amos Makalla akiwajibu wabunge
waliotaka kujulishwa faida za mwenge na bajeti yake kwa mwaka, alisema falsafa
yake ni kuwaletea wananchi nuru palipokuwa na giza, kuheshimiwa na kukombolewa.
Mbunge
wa Simanjiro Ole Sendeka aliomba muongozo akidai Mwenge huo ambao ni alama na
tunu ya taifa kuleta tumaini pale ambapo hapana matumaini kwa wale wanaojua
historia. Alisema kwa kuwa kuna uelewa mdogo kwa Watanzania juu ya jambo hilo
huku wengine wakijipenyeza na kuingia ni bora ofisi ya Bunge ikatoa elimu.
0 Response to "HIVI NI KWELI MWENGE WA UHURU UNACHOCHEA MAAMBUKIZI YA UKIMWI?"
Post a Comment