Muonekano
mzuri kimavazi na haiba, kwa Kiswahili kisichokuwa rasmi siku hizi maarufu kama
‘Kutokelezea’ kunaweza kukuongezea kipato chako. Kwa mujibu
wa makala moja kutoka Jarida la Forbes (isome yote hapa ukitaka) Mwandishi David
K. Williams anasimulia……………
Watu watanashati na waliofanikiwa huonyesha umaridadi wao katika kila jambo wanalolifanya. Hata hivyo siyo kila siku mtu unahitaji muda, pesa na umakini katika shughuli rasmi za kikazi, utamaduni wa makampuni hutofautiana. Kwa mfano sisi kwenye kampuni yetu tunavaa Jeans na Tshirt. Tunajisikia vizuri tu, tunaweka kipaumbele katika afya na mazoezi na uvaaji usiokuwa rasmi hutusaidia katika kupangilia mambo yetu vizuri, kuuza vizuri nk.
Kila mtu
anaweza kunufaika kutokana na kujifunza kidogo kuhusu namna ya kujiweka vizuri mwenyewe
katika ulimwengu wa mafanikio. Mtaalamu wa mitindo na mavazi Lindsay Shores
anaweka wazi njia za kutumia katika kuongeza mafanikio kwenye kazi na biashara
kwa kuzingatia muonekano wetu mbele za watu.
“Yeyote
anayesema ‘Ni kile kilichomo ndani
ndicho kinacho’matter’ (muhimu)’, hayuko
sahihi” anasema Lindsey. “Lakini kile kilichokuwa nje kinaweza kikawa muhimu
zaidi. Mitindo siku hizi inasonga mbele kila kona”
Mbali na
kubainika kwamba kuvaa vizuri kunaweza kuongeza kipato, pia ni muhimu katika kuongeza heshima ya mtu binafsi na
haiba yake. Mwandishi mwingine mashuhuri, M.Mafiso anasema, kuna njia 7 za
kupata heshima. Ya kwanza anasema, “Pasipokujali zamani ulifanya kitu gani,
wewe ni tajiri kiasi gani, umaarufu wako au hata umbile lako kama ni mnene au
mwembamba, lakini ukiwa umevalia vizuri
mara zote utatendewa vizuri kuliko yule aliyevalia kawaida.
![]() |
Mwanamitindo Lindsey Shores siku ya harusi yake. |
Mantiki yake
inafanya kazi katika nyanja zote za biashara, iwe ni kwa mwanamuziki, mpokea
wageni, na hata mcheza golf. “Valia vizuri kwenye pati, pasipokujali ni pati ya
namna gani kwani ni muhimu katika kufikisha ujumbe kwamba,wewe ni nani na
unataka kuwa nani. Na jambo hili linatakiwa liwe ndiyo kitu cha kwanza katika
akili yako kila asubuhi unapoamka” anasema Lindsey. “Kuvalia vizuri mahali pa
kazi , kunakuongezea tabia za uchangamfu pamoja na kuzidisha kujiamini”.
Katika
biashara ni ukweli usiopingika kuwa, “kamwe
huwezi kupata tena kwa mara ya pili nafasi ya kuonyesha muonekano wako mzuri wa
kwanza”
0 Response to "KUVALIA VIZURI HUONGEZA KIPATO."
Post a Comment