INDIA
India imeunda
meli yake ya kwanza yenyewe iliyokuwa na uwezo wa kubeba ndege na vyombo vya
angani katika mji wa Kusini wa jimbo la Kerala.
INS Vikrant. |
Ripoti
inasema kuwa meli hiyo yenye uzito wa tani 37,500 inayoitwa INS Vikrant
inatarajiwa kufanyiwa majaribio makubwa mwaka 2016 kabla haijaungana na
meli nyingine za kijeshi mwaka 2018.
Nchi
nyingine zenye uwezo wa kuunda meli kama hiyo ni Marekani, Uingereza, Urusi na
Ufaransa. Meli hii ina urefu wa mita 260 sawa na futi 850 na upana wake ni mita
60. Imeundwa bila kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi kwa kutumia
chuma aina ya steel chenye ubora wa hali ya juu kutoka kampuni inayomilikiwa na
serikali.
CHANZO : BBC NEWS
0 Response to "MELI UKUBWA WA VIWANJA 2 VYA MPIRA YAUNDWA INDIA."
Post a Comment