VATICAN CITY
Papa Francis
binafsi ametoa salamuza Eid El Fitr kwa Waislamu wote duniani, baada ya
kuhitimisha Mwezi mtukufu wa Ramadhani huku akiwahimiza kuheshimiana baina ya
Dini zote.
Salamu kama
hizi kwa kawaida hutolewa kila mwaka na Vatican lakini tofauti ni kwamba miaka mingine
hutolewa na Baraza la Kipapa la mijadala ya kiimani.Hii ni mara ya pili kwa
ujumbe binafsi kutolewa na papa tangu mtangulizi wake Papa Yohane Paul II mwaka
1991.
Alitoa wito
wa kudumisha kuheshimiana kwa njia ya kutoa elimu. Huku mivutano ya kikanda na
kidini ingali ikishika kasi kote duniani, Papa amehimiza umuhimu wa
kuheshimiana na umuhimu wa kuwaelimisha vijana wa Kiislamu na Kikristo juu ya
upendo na kuheshimiana.
“Sote
tunafahamu kuheshimiana ni jambo la msingi katika mahusiano yeyote yale ya
binadamu hasa miongoni mwa watu wanaohubiri imani za dini. Kwa njia hii,
urafiki wa kweli na wa kudumu unaweza kukua. Ujumbe wangu kwenu mwaka huu ni
kuwataka nyote Waislamu na Wakristo kuakisi matendo yenu ya kiimani na
kudumisha ushirikiano na kuheshimiana” Alisema Papa.
0 Response to "PAPA FRANCIS ATOA SALAMU ZA EID EL FITR KWA WAISLAMU WOTE DUNIANI."
Post a Comment