UTAJIRI WA WASANII, DIAMOND, WEMA, NA MASANJA MKANGAMIZAJI UNATIA SHAKA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UTAJIRI WA WASANII, DIAMOND, WEMA, NA MASANJA MKANGAMIZAJI UNATIA SHAKA


Yadaiwa ni wa madawa ya kulevya.


Hivi karibuni kumeibuka tetesi nyingi kuhusiana na majina ya  watu wanaojihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya. Miongoni mwa watu waliohisiwa wapo wabunge, wafanyabiashara,  viongozi mbalimbali wa dini na sasa wameanza kuhisiwa wasanii wa filamu na muziki  hasa baada ya wasanii Agness Gerald “Masogange” na Mellisa Edward kukamatwa na dawa hizo huko nchini Africa ya Kusini.
Diamond
Kwa mujibu wa gazeti pendwa la Visa wiki hii, Msanii Diamond, anahisiwa labda anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya  kutokana na mafanikio yake makubwa kiuchumi aliyoyapata ndani ya muda mfupi ukimlinganisha na wasanii wengine ambao kazi zao ni nzuri lakini hawana kitu. Wasanii wengine ambao mafanikio yao kiuchumi yameonekana hayawezi yakalingana na kazi  au umaarufu waliokuwa nao ni Wema sepetu na Masanja Mkandamizaji.


Wema Sepetu 
Imedaiwa kwa mfano, Wema  Sepetu licha ya kutoa filamu ambayo hata mtaani haikuweza kuonekana kwa wingi na akadai kutumia mamilioni ya pesa kuiandaa watu wameshangazwa na ukwasi wake na jinsi anavyojitolea kuchangia maswala mbalimbali ya kijamii mfano ni pale alipomtolea faini msanii mwenzake Kajala Masanja asiende jela. Masanja Mkandamizaji au Emanue Mgaya , yeye anadaiwa kuwa na safari nyingi za nje pamoja na kumiliki vitu vingi vya thamani ikiwemo jumba la ghorofa tofauti kabisa na ilivyo  kwa wasanii wenzake kutoka kundi moja.

Hata hivyo, hizi ni tuhuma tu na hisia za watu ambazo bado hazijawa na uthibitisho wowote ule, na gazeti la Visa lilipowasiliana na wasanii hawa simu zao zilikuwa zikiita pasipo kupokelewa.

'Masanja Mkandamizaji'
Wakati huo huo, Msanii na msambazaji wa filamu za kibongo Wiliam Mtitu ameliambia Visa kwamba, pamoja na  kukutana na vikwazo vingi katika usambazaji wa filamu, atahakikisha anapambana mpaka dakika ya mwisho na kwamba hatakata tama hata kidogo.   “Huu ni wakati wetu sisi  wazawa kuanza   kusambaza  filamu zetu wenyewe badala ya kuwategemea wawekezaji” Alisema Mtitu.

CHANZO: Gazeti la Visa.

0 Response to "UTAJIRI WA WASANII, DIAMOND, WEMA, NA MASANJA MKANGAMIZAJI UNATIA SHAKA"

Post a Comment