DAR ES SALAAM, Tanzania
MWENYEKITI wa Kampuni za IPP,
Reginald Mengi,amesema vijana wanaosubiri mifumo iliyowekwa iwasaidie
kujikwamua kiuchumi wataendelea kubaki kuwa watumwa wa maamuzi ya watu wengine.
Mengi alitoa kauli hiyo jijini Dar
esSalaam, leo wakati akikabidhi zawadi kwa washindi watatu walioshinda shindano
la wazo bora la 'kutweets na Mengi'.
Amesema kwa sasa vijana wengi
wanamaliza elimu ya msingi Sekondari na vyuo vikuu ambao hawana ajira wala
mitaji na wengi wao wanajisikia kama hawana pa kutokea.
Aliongeza kuwa licha ya
serikali, jamii na wazazi kuwa na wajibu katika jambo hili kijana anapaswa kuwa
mtu wa kwanza kutafuta njia inayowezekana kwake.
Swali la mwezi julai lililowatoa
washindi hao liliuliza “Kijana asiyekuwa na ajira wala fedha anawezaje kuanza kujijenga
kiuchumi”ambapo Tony Alfred muuza kahawa katika kituo cha mabsi Ubungo aliibuka
mshindi wa kwanza.
Alfred ambaye ni msomi wa shahada ya
masoko kutoka chuo kikuu cha Da resSalaam, aliwashinda John Mkungu na Maduhu
Jumanne kwa jibu lake lililoeleza kuwa “kama kijana fikiria katika hali uliyopo
ni nini unachoweza kufanyia jamii yako, ukipata jibu huo ndio mtaji na ajira
yako.”
Kutokana na ushindi huo Alfred
amejipatia Sh Mil 1 ambapo John Mkungu alishika nafasi ya pili na kujipatia
kiasi cha Sh laki 5 na maduhu jumanne alijipatia sh. laki 3
Mengi aliongeza kuwa kutokana na
watu wengi kuchangia katika mtandao wake wa kijamii wa Tweeter, ataanda mpango
wa kuyakusanya mawazo yaliyokuwa mazuri na kuyaweka katika mfumo sahihi kisha
kuyafikisha kwa vijana wengine kupitia mashuleni na vyuoni.
Akizungumzia ushindi wake Alfred
alisema Alfred alimshukuru Mengi kuanzisha mfumo huo na kuwataka vijana wenzake
wasikate tamaa pale wanapokosa ajira za serikali.
Kumbuka hapo May 13 mwaka huu Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi alianzisha shindano la ku 'Tweet' ambalo litakuwa likifanyika kilamwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja na mshindi wa kwanza atakayeandika tweet bora juu ya kupigana vita dhidi ya umasikini atajipatia sh. millioni moja. Kwa habari zaidi juu ya shindano lililopita tembelea
VYANZO : Blogu ya Hakingowi na mtandao wa IPP Media.
0 Response to "“Vijana wanaosubiri mifumo iliyowekwa iwasaidie kujikwamua kiuchumi wataendelea kubaki kuwa watumwa wa maamuzi ya watu wengine.” -Dr. Mengi."
Post a Comment