Mtu wa pili
kwa utajiri nchini China amejeruhiwa kwa kile kinachoelezwa kwamba ni ulipizaji
kisasi kwa mfanyakazi aliyetimuliwa kazi.
Billionea
huyo, Zong Qinghou (67) na kampuni yake iitwayo ‘Wahaha’ ndiye anayeongoza
katika biashara ya vinywaji nchini humo. Jarida la Forbes linakisia utajiri
wake kufikia Dolla za Kimarekani billion 11. Tajiri namba moja nchini China ni
Wang Jianhii mwenye utajiri unaofikia dolla billion 14.
Alishambuliwa
siku ya ijumaa karibu na nyumbani kwake,
na kujeruhiwa vidole vya mkono wake. Mtuhumiwa tayari amekwisha kutiwa mbaroni
na polisi wa huko huko Uchina.
Chanzo: AL
Jazeera.
0 Response to "BILLIONEA NAMBA 2 CHINA AJERUHIWA KULIPIZA KISASI"
Post a Comment