Kufanyiwa majaribio kwa binadamu hivi karibuni
Virus wa Ukimwi |
Chanjo kwa Nyani inayofanana naya Ukimwi
kwa binadamu imeonyesha kutokomeza kabisa virusi, utafiti umeonyesha. Utafiti
uliochapishwa katika Jarida la ‘Journal Nature’
umeonyesha kwamba Nyani waliochanjwa wanaweza wakamaliza kabisa virusi
wanaodhoofisha kinga ya mwili wajulikanao kama SIV Mac 239 kutoka miili yao.
Ilifanya kazi vizuri kwa Manyani 9
kati ya 16 waliochanjwa . Wanasayansi wa Kimarekani wamesema kwamba wanataka
kutumia njia kama hiyo kufanya majaribio ya chanjo ya HIV kwa Binadamu. Profesa
Lous Picker kutoka Chuo kikuu cha Tiba cha Oregon amesema; “Ni vigumu kudai
virusi vimetokomea kabisa , inawezekana kuna seli ambazo labda hazikuchunguzwa
vizuri zilizobaki na virusi, lakini kwa sehemu kubwa kulikuwa hamna kirusi
kilichosalia katika miili ya nyani hao”
Virusi hao aina ya SIV Mac 239 ni
hatari mara 100 kuliko vile vya HIV. Nyani aliyeathirika hufa ndani ya miaka 2.
0 Response to "CHANJO YA UKIMWI YAMALIZA KABISA VIRUSI NDANI YA SOKWE"
Post a Comment