Tuko majirani katika shughuli zetu za kila siku, lakini
mpaka nakuja kujua kwamba kijana huyu ni msanii mwimbaji wa Bongo fleva au
tuseme hip hop kama yeye mwenyewe anavyo sema ni baada ya kumuuliza juu ya
wimbo mmoja ambao nilikuwa nikiusikia ukipigwa sana redioni, ‘Nipe love’ kwamba
ni nani aliyeupiga.
|
Jefryder akifanya shooting ya wimbo wake 'Nipe mic' |
Kwa hakika wimbo huu mimi binafsi naupenda mno, na
nilishangaa sana aliponiambia kwamba ni wimbo wake. Jafary Ahmed au kwa jina la
usanii ‘JEFRYDER’ ni kijana aliyeamua kujiajiri mwenyewe kupitia sanaa ya
muziki wa kizazi kipya hususan Hip Hop. Mpaka sasa hivi ameshatoa ngoma kali
mbili, hii ya Nipe love na nyingine ambayo amenieleza ni jana tu amemalizia
kufanya video yake inayokwenda kwa jina la NIPE MIC. Anasema “ Inshaalah Kwa Rehma za Mwenyezi Mungu, Muumba
wa vyote, video hiyo inaweza ikaanza kurushwa hewani mwanzoni mwa mwezi Oktoba”
|
Jefryder katika shooting ya Nipe mic |
Kijana Jefryder anachoomba kwa wadau wote wa muziki ni ‘support,’ anasema angefurahi sana endapo
atapata watu wa kumfadhili ili aweze kutimiza malengo yake katika muziki ikiwa
ni pamoja na gharama mbalimbali za kurekodi pamoja na kufanya shooting za video
za nyimbo zake. Anasema anazo track nyingi ambazo tayari ameshaziandaa lakini
kikwazo ni gharama. Ikiwa atapata sapoti ya kutosha anasema atatoa album
itakayomtambulisha vizuri zaidi.
|
Jeff akiendelea kuchana mistari |
Hapa chini ni ngoma zake mbili Nipe Love na ya pili ni Nipe
Mic, zisikilize ni nzuri kwa kweli.
0 Response to "JEFRYDER NA NGOMA NIPE LOVE, NIPE MIC, MJASIRIAMALI WA HIP HOP ANAYEKUJA KWA KASI"
Post a Comment