Mbunge wa Mbeya mjini Mh.Joseph Mbilinyi au ‘Sugu’
amesema kwamba Naibu Spika, Mheshimiwa
Job Ndugai alilinajisi Bunge kutokana na kitendo chake cha kuita askari ambao
hawaruhusiwi kuingia ndani ya Bunge kikanuni, na taratibu na kisheria.
Vurugu zikifanyika Bungeni |
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na idhaa ya Kiswahili
ya redio Ujerumani DW kuelezea kwa ufupi kile kilichotokea siku ya tarehe 5
Alhamisi wiki iliyopita.
Alisema kwamba, Waziri Lukuvi ambaye ni mwakilishi wa
serikali Bungeni na Mwanasheria Mkuu walikuwa wameshapewa dakika 40 kuelezea
mambo yao, lakini Kiongozi wa upinzani Bungeni alipojaribu kutafuta nafasi ili
atoe ufafanuzi kwa faida ya Taifa, Naibu spika alikuwa mkali na kumzuia kwa
kuwa alijua anachokifanya.
“Baada ya kumzuia, haijapita hata dakika 2 anaanza kuita
askari, na siyo tu askari wa Bunge, siku ile Bunge lilinajisiwa kwa maana
kwamba aliruhusu askari ambao hata wanje…” Alisema.
Aliendelea kusema kwamba, Wabunge wote wa upinzani
wakiwemo NCCR, CUF na CHADEMA waliamka na kwenda “kumprotect” mwenyekiti wao
asidhalilishwe kitoto namna ile lakini kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe
Naibu spika, alimlenga Sugu tu na kuamuru akamatwe na atolewa nje.
Akitolea ufafanuzi juu ya jina lake la utani ‘Sugu’ alisema Watanzania wanaelewa maana yake ni
nini, na wala siyo kwamba lina maanisha ni mkaidi. “Sugu siyo sugu ya kupigana
ngumi, sugu ni sugu ya kung’ang’ania kitu, kukomalia kitu, yaani ninapoona kitu
hakipo sawa huwa sikubali kilaini”. Alimalizia Mheshimia Sugu.
0 Response to "JOSEPH MBILINYI ‘SUGU’ ASEMA BUNGE LILINAJISIWA"
Post a Comment