MAONI YANGU.
Uhalifu unaoendelea nchini hususani
visiwani Zanzibar ungeweza kupungua kwa kiwango kikubwa au kumalizika kabisa
endapo zingeliwekwa kamera maalumu mitaani za cctv (videosurveillance systems) ambazo huweza kuwanasa 'live' watuhumiwa wakati wakitekeleza unyama wao.
Mataifa yaliyoendelea ni nadra sana kukuta
kitendo kama cha kumwagia mtu tindikali tena hadharani kushindikana kujulikana
waliotenda. Nchi kwa mfano Uingereza
serikali za miji mbalimbali zinanaweka bajeti kubwa sana kwenye mifumo hii ili
kuweza kukabiliana na uhalifu wa namna hii.
Sasa matukio hayo yenye sura ya kigaidi yamefika zaidi ya 8,
huku jeshi la polisi likidai linafanya uchunguzi. Kuna tukio hili la padre wa
kanisa katoliki Padri Joseph Onesmo mwangamba aliyemwagiwa tindikali, Sheha wa
Mohamed Omar Said wa Tomondo naye alimwagiwa tindikali, Padri tena wa Kanisa
katoliki Parokia ya Mtoni mjini Magharibi padre Evaristi Mushi yeye aliuwawa kwa risasi.
Padre Ambros Mkenda naye alijeruhiwa
vibaya kwa risasi, mmiliki wa Home shopping centre Said Mohammed Saad jijini Dar alimwagiwa tindikali, wasichana Kate Gee na
Kristie Trup wote raia wa Uingereza waliomwagiwa tindikali na kuumia maeneo
mbalimbali miilini mwao, Katibu wa Mufti
Zanzibar Shehe Fadhil Sulleiman Soraga aliyejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa
tindikali usoni, na matukio mengine ni
milipuko ya mabomu katika mkutano wa chama cha CHADEMA na sherehe za uzinduzi
wa parokia kanisa katoliki Olasiti.
Pamoja na uchunguzi huo serikali inaodai
unaendelea lakini mpaka sasa hivi hakuna mtuhumiwa yeyote aliyetiwa hatiani na
mahakama au kubainika kwa uhakika kabisa ni mtandao gani au kikundi kinachojihusisha
na njama hizo au wana sababu zipi zinazowasukuma kutenda matendo hayo
yaliyokuwa kinyume kabisa, siyo tu na haki za binadamu, bali hata na dini yeyote ile chini ya jua
inayomtaja Mwenyezi Mungu.
0 Response to "KAMERA ZA CCTV ZINGELIWEZA KUKOMESHA UNYAMA HUU"
Post a Comment