Afisa mtendaji mkuu wa microsoft Steve Ballmer, kusoto na Mwenyekiti wa bodi, Nokia, Risto Siilasmaa kulia |
Kampuni ya simu za mkononi ya Nokia imesaini mkataba wa kununuliwa
na Kampuni kubwa la Microsoft kwa kiasi
cha shilingi trilioni 11.5 sawa na Euro bilioni
5.4 au dola bilioni 7.2.
Nokia pia itatoa leseni zake za hati
miliki pamoja na ramani za huduma zake kwa kampuni hiyo inayomilikiwa na tajiri
namba moja Marekani Bill Gates.
Kwa mujibu wa mitandao mbali mbali ikiwemo
Sky News, BBC, CNN na USA Today,
Makampuni hayo kwa pamoja yalinukuliwa mbele ya waandishi wa habari kuwa makubaliano
hayo yatakamilika mwanzoni mwa mwaka ujao, wakati ambao kiasi cha wafanyakazi
32,000 wa Nokia watahamishiwa kwenye kampuni ya Microsoft.
Wakati Nokia ikikumbwa na
ushindani mkali kutoka kwa washindani wake Samsung& Apple na simu zao za kisasa za smsrtphones yenyewe imeendelea kubakia nyuma na simu zake za bei ya chini kama nokia za tochi. Vilevile imekuwa
ikikosolewa kwa kutokuwa na kasi ya kutosha kwenye soko la simu za mikononi.Kwa upande mwingine Samsung na Apple nao wamekuwa wakikosolewa vikali kutokana na simu zao pamoja na vifaa vingine kama Ipad na kompyuta mpakatoto kutokukaa na chaji muda mrefu. Ikiwa Microsoft watakuja na ubunifu betri ikakaa angalao siku mbili au tatu washindani wake hao watakuwa wamepigwa bao la kisigino. Si ajabu nao wakaja na aina nyingine mpya ya smartphones.
“Ni hatua kubwa kwa siku zijazo ambapo ni mafanikio makubwa kwa wafanyakazi, wanahisa na wateja wa makampuni yote mawili” alisema Steve Ballmer, Mtendaji Mkuu wa Microsoft.
0 Response to "KAMPUNI KUBWA LA MICROSOFT 'LAIMEZA' NOKIA"
Post a Comment