Eneo la Turkana lenye ukame mkubwa |
Serikali
ya Kenya imetangaza ugunduzi wa visima vikubwa vya maji chini ya ardhi ambavyo
vinaweza kumudu mahitaji ya maji katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini
ijayo katika jimbo la Turkana na kwa nchi nzima.
Visima
hivyo bila shaka vitaleta afueni kwa wakaazi kwani Turkana ni eneo kame
Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Eneo hilo pia lina viwango vya juu vya
umaskini.
Ugunduzi huo ulitokana
na utafiti wa wanasayansi waliotumia teknolojia ya satellite
Visima hivyo vinapata
maji kutoka kwa chemichemi za maji kutoka milima ya mbali kwa hivyo maji yake
yakitumiwa vyema huenda havitawahi kukauka.
Mamilioni ya wakenya
wanakosa maji safi.
Nchi hiyo pia
inakabiliwa na msimu tata wa mvua na inakabiliwa na athari za mabadiliko ya
tabia nchi.
Utafiti ulifanywa na
shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO na wanasayansi wa Kenya kwa ufadhili wa
serikali ya Japan.
0 Response to " Kenya yagundua visima vikubwa vya maji chini ya ardhi"
Post a Comment