Tabia ya
binadamu ya kugawana vitu imeanza zamani kuliko ilivyokuwa imefikiriwa hapo
kabla. Imeanza tangu alipokuwa na umbile kama la sokwe. Katika utafiti
uliofanyika na kuchapishwa katika jarida la Academy of Science kutaka kugundua
ni kwa nini binadamu hugawana vitu, ilibainika kwamba kumbe tabia hiyo hata
sokwe nao wanayo tena sawasawa kabisa na ilivyokuwa kwa binadamu.
Sokwe mmoja
alipopewa vidude mkononi alimgawia mwenzake sawa sawa nay eye mwenyewe,
hii inamaana kwamba hata wanapopewa ndizi hufanya hivyo. Utafiti huu ulibaini
kuwa sokwe wana tabia ya kugawana hata chakula sawa kwa sawa na ikitokea mmoja akampunja mwenzake huyo
aliyepunjwa hugoma kabisa kupokea.
Wote
binadamu na sokwe wanatabia zinazofanana katika kugawana vitu, huwinda pamoja,
hugawana vyakula, husaidiana katika kulea watoto nk.
Chanzo BBC.
Chanzo BBC.
0 Response to "KUMBE SOKWE HUGAWANA VITU SAWA KAMA BINADAMU."
Post a Comment