Sayari ya Mars |
Hivi karibuni mwaka 2011 iliibuka Taasisi moja isiyokuwa ya
kiserikali inayojiita MARS ONE na kudai kwamba ina malengo ya kuhakikisha mpaka
ifikapo mwaka 2022 iwe imeshapeleka watu wane kuishi katika
sayari ya Mars na itaendelea na kupeleka wengine kidogokidogo.
Ikumbukwe kwamba Baada ya mashindano ya Wamarekani na Warusi miaka ya 60 na 70
kupeleka vyombo mbalimbali na watu katika anga za juu Marekani hatimae walifanikiwa kuwa wa kwanza kupeleka chombo katika sayari
ya Mars lakini kisichokuwa na binadamu ndani mnamo June 19 mwaka 1976, chombo
hicho Viking 1 kilikuta uwezekano wa binadamu kuishi pale haupo kabisa kutokana
na hali ya hewa kuwa baridi mno na hamna maji.
Wamarekani hao hao tena wakawa wakwanza kupeleka binadamu wa
kwanza akatua katika uso wa mwezi mnamo
July 20 1969 wakiwa na chombo kilichoitwa Apollo 11.
Sputnic satelite ya kwanza angani |
Mpaka sasa hivi
Shirika la NASA lA Marekani na hata nchi nyinginezo kama Uchina,
wanaendelea na misheni mbalimbali anga
za juu kutafuta uwezekano wa binadamu kwenda kuishi huko, au hata kujua kama
kuna viumbe wenye uhai wanaoishi katika sayari nyingine tofauti na dunia hii
lakini hamna dalili yeyote zaidi ya Mars kuonekana kama iliwahi kuwa na maji
miaka mingi iliyopita lakini haijabainika bado yalikokwenda ni wapi.
Viking 1 chombo cha kwanza kutua Mars |
Hali hii inafanya uwezekano wa Binadamu kwenda kuishi Sayari
ya Mars kuwa mdogo sana na hata hii
taasisi ya Mars One huenda ina agenda zake nyinginezo kama vile kujikusanyia
fedha kiujanja na siyo kuwapeleka watu wakaishi Sayari ya Mars kama inavyodai.
Lakini pia hatuwezi tukapinga kabisa uwezekano huo kwani ikiwa vitatengenezwa vyombo maalumu mfano wa Apollo na ambavyo vitawekewa mazingira ndanio yake yanayofanana na humu duniani basi jambo hilo litawezekana. Hata hivyo kitu kama hicho ni gharama kubwa sana, na pengine hata yachange Mataifa makubwa mawili au matatu haitakuwa rahisi hata kumuweka binadamu mmoja pale kwa masaa, sembuse kwenda kushika kiwanja kule cha kulima.

Chanzo, mitandao mbali mbali ikiwemo, WIKIPEDIA, na MARS ONE
0 Response to "MAISHA SAYARI MPYA YAJA, JIANDAE"
Post a Comment