HUU NI MTAZAMO WANGU:
Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete |
Ni dhahiri
kabisa sasa kwamba Uganda , Rwanda na Kenya , siyo kitu kimoja tena na Tanzania
kama ilivyokuwa wakati walipoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki. Badala yake
kinachoonekana kinafanana na kile kilichoiua Jumuiya ya Africa Mashariki ya
akina Mwalimu JK.Nyerere, Idd Amin Dada na Jommo Kenyata hapo mwaka 1977; ‘tofauti
za viongozi kuliko wananchi wa kawaida’.
Mimi binafsi
naona kinachowasumbua Maraisi hawa wa nchi hizi tatu ni wivu, ukiwachunguza wote, Kagame, Museven na Kenyatta , wote wana “Majanga”
aidha yanayowasubiri au yanayowasumbua tayari kwa muda mrefu.
Tukianza na
Museven, yeye kwanza amengangania madaraka kwa muda mrefu kitu ambacho hata
waliokuwa washirika wake wa karibu sana nchi za Magharibi zimeanza kumchoka.
Licha ya kuitisha chaguzi za mara kwa mara lakini kidemokrasia ilifaa angatuke.
Kutokana na sababu hii wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanamweka katika kundi
la akina Muamar Ghadafi na Mubarak. Kutokana na sababu hizo bila shaka atamuona
Rais Kikwete kama yuko juu zaidi yake.
Kwa upande
wa Rais Paul Kagame, yeye kama rafiki yake Museven, amengangania madarakani kwa
muda mrefu na inadaiwa pia kwamba anawakandamiza wapinzani wake kisiasa na hata
wakati mwingine kutuma majasusi kwenda kuwaulia uhamishoni wanakokimbilia kwa
kisingizio cha kutokomeza ubaguzi wa kikabila. Janga jingine linalomuandama ni
hili la “kutia mafuta ya taa” mgogoro Mashariki mwa DRC, Wachambuzi wamefika
mbali na kutabiri hata Kagame kuja kuburuzwa The Hauge siku za usoni kama kina
Loraa Gbagbo na Charles Tylor.
Rais Kenyata,
kwanza anashangaza kwani, Kikwete ndiye aliyekwenda kusaidia kupoza machafuko ya
ghasia za baada ya uchaguzi 2007 pasipo
kuonyesha kuegemea upande wowote. Kenyata pamoja na kushinda uchaguzi uliopita
, lakini bado suala la kesi yake na Ruto ICC nalo linamfanya ajione mdogo mbele
ya Jk.
“Majanga”
hayo ya Maraisi hawa watatu yanawakosesha usingizi na kumuona mwenzao Rais
Kikwete kama ana bahati na yupo juu zaidi kuliko wao. Ujio wa Viongozi wakubwa
wakubwa wakiwemo Maraisi wa Marekani hasa Rais Barak Obama kulizidi kuwachefua
, kwa kuona hata endapo hapo baadae labda Marekani itaamua kumng’oa mmoja wao
kama ilivyofanya kwa kina Ghadafi basi ni lazima iitumie Tanzania kama ‘Base’
Sasa ndio
wameamua kumzunguka kwa visingizio kibao visivyokuwa na kichwa wala miguu ili Jk na Tanzania kwa ujumla tuonekane hatufai
mbele ya jumuia za Kimataifa.
0 Response to "'MAJANGA' YA MARAISI AFRIKA MASHARIKI CHANZO CHA WIVU KWA JK."
Post a Comment