"Papaa Msofe, Aurora waongoza jeshi"
Baada ya sifa ya Tanzania kuingia doa kutokana na watu
wengi maarufu kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya , uchunguzi wa JAMHURI
umebaini kuwa matajiri wengi nchini wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kutupwa kwa
Wazungu kupitia ahadi hewa za kuwauzia madini.
Taarifa nyeti zilizonaswa na JAMHURI zinaonyesha
uchunguzi wa kina uliofanywa na serikali umebaini uwepo wa wafanyabiashara
wenye leseni halali za udalali wa madini, lakini biashara wanayofanya ni
kuwatapeli Wazungu kisha wanatembeza rushwa kwa baadhi ya Polisi na Mahakama kukatish tama Wazungu waliotapeliwa.
“Ndugu zangu nawaambia
watu hawa hawana woga kabisa. Majina haya unayoyaona Wizara imefikia uamuzi wa kuyapeleka kwa
Mheshimiwa Rais(Jakaya Kikwete), pengine aingilie kati na kuzilazimisha mahakama na hawa polisi
kuhakikisha wahusika wanakamatwa...jina la Tanzania linanuka nje ya nchi sababu
ya watu hawa “ kilisema chanzo chetu.
Baada ya kupata orodha ya majina haya , JAMHURI kwa
nyakati tofauti liliwasiliana na matajiri wanaotuhumiwa mmoja baada ya mwingine
kwa kutumia barua pepe na simu zao za mkononi, na mchezo ukawa ule ule jinsi
wanavyowatapeli Wazungu.
Hawa wana utajiri mkubwa ajabu,. Wanaingia kwenye
mtandao na kuwadanganya Wazungu kuwa wana madini hadi kilo 600, wanawatumia
vivuli vya leseni zao halali walizozipata kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
kisha Wazungu wanaamini kuwa ni biashara halali, na wanapotuma fedha tu
zinaondolewa kwenye akaunti mara moja.
Mtandao huu ni mpana kwani unahusisha baadhi ya
watumishi wa benki za hapa Tanzania na nje ya nchi ikiwamo Marekani na
Australia, ambako mabillioni ya fedha yanaingizwa kwenye akaunti kwa njia ya
utapeli na kuondolewa haraka. Wahusika wanamiliki magari ya kifahari na
wanajenga maghorofa.
Maeneo yaliyokithir katika utapeli wa madini ni Dar es
salaam, Arusha na Mwanza. Waraka
ulioonwa na Jamhuri unaokwenda kwa Rais unaonyesha kuwa vitendo vinavyoendelea
sasa hivi vya utapeli katika biashara ya madini vinaichafua sifa ya Tanzania na
kuikosesha serikali mapato yanayotokana na biashara ya madini.
Ukitaka kuisoma habari hii nzima pamoja na majina ya Matajiri
wanaotuhumiwa utaipata katika Gazeti la
JAMHURI toleo la leo Septemba 3.
0 Response to "MATAJIRI MATAPELI TANZANIA HADHARANI"
Post a Comment