MJI WA KALE UKRISTO ULIKOANZIA WASHAMBULIWA VIKALI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MJI WA KALE UKRISTO ULIKOANZIA WASHAMBULIWA VIKALI

Mapambano katika mji wa kale wa kikristo huko Syria yanaendelea, licha ya ripoti kwamba vikosi vya serikali vilikuwa vimeushikilia.

Mwakilishi wa BBC nchini Syria Jeremia Bowen amesema mapigano makali na waasi yalikuwa yakiendelea mjini Maaloula huku moshi ukionekana ukipaa angani.

Mji wa kale wa kikristo wa Maaloula
Aliongeza kuwa bado alikuwa hajapata ushahidi wa Alqaeda  kuharibu maeneo muhimu ya ukumbusho wa kidini. Tangu kuanza kwa mapambano hayo raia zaidi ya 3,300 wameuhama mji huo kwenda maeneo salama yakiwemo Damascus.

Wakazi hao wamedai kundi la Al Nusra  lilikuwa limeharibu Makanisa na sanamu. Mji wa Maaloula una Makanisa kadhaa na Monasteri muhimu ikiwemo Deir Mar Takla ambayo hutembelewa na mahujaji wengi wa Kikristo nma Kiislamu.
 
Mapambano yakiendelea

Maandiko yaliyopatikana kutoka katika baadhi ya mapango upande upande wa mlima mji ulipokaa yameuthibitisha mji huo kuwa moja ya vituo vya mwanzo kabisa vya Kikristo duniani, na hata baadhi ya wakaazi wake bado wanaweza kuzungumza lugha ya Aramaic ambayo ndiyo aliyokuwa akizungumza Yesu Kristo enzi zake.

0 Response to "MJI WA KALE UKRISTO ULIKOANZIA WASHAMBULIWA VIKALI"

Post a Comment