Michel Djotodiam Rais aliyenyakua madaraka |
Mkuu wa jeshi la
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, amefutwa kazi baada ya wapiganaji wanaomuunga mkono
rais aliyeondolewa mamlakani kuanzisha mapigano mapya.
Kwa
mujibu wa mafisa wakuu, angalau watu 60 wameuawa kwenye mapigano hayo Kaskazini
Magharibi mwa mji mkuu
Muasi wa zamani Michel
Djotodiam, aliapishwa kama rais mpya wa nchi hiyo mapema mwezi huu baada ya
wanajeshi kumwondoa mamlakani,
Francois Bozize mwezi Machi.
Francois Bozize mwezi Machi.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa
Jamuhuri ya Afrika ya Kati huenda ikawa taifa lililoporomoka na hata kutishia
amani katika kanda hiyo.
Takriban
thuluthi moja ya watu 4.6 raia wa nchi hiyo, wanahitaji msaada wa chakula ,
makaazi , huduma za afya na maji.
Wanajeshi wanaomuunga mkono
bwana Bozize wanasemekana kutwaa angalau mji mmoja tangu kuanza mashambulizi
yao wiki jana.
Hii ndiyo operesheni ya kwanza
kubwa wanajeshi wafuasi wa rais wa zamani wameweza kufanya, tangu kuondolewa
mamlakani.
Nafasi ya Jean-Pierre
Dolle-Waya kama mkuu wa majeshi itachukuliwa na Generali Ferdinand Bombayake,
kulingana na taarifa iliyosomwa katika redio ya taifa.
Gen Bombayake alikuwa mkuu wa
usalama wa rais wa zamani, Ange Felix Patasse, aliyeondolewa mamlakani mwaka
2003 kwa njia ya mapinduzi na bwana Bozize.
Wafanyakazi
wa mashirika ya kibinadamu, wametuhumu wapiganaji wa zamani wasio na maadili
kwa kupora mfumo wa afya pamoja na kuwaibia raia tangu waasi wa Seleka kuchukua
mamlaka mwezi Machi.
0 Response to "Mkuu wa Majeshi atimuliwa kazi"
Post a Comment