![]() |
'Makanisani na Misikitini' |
Hayo yamesemwa leo asubuhi na Katibu Mkuu wa Shirika la linalojishughulisha
na uzuiaji wa matumizi ya dawa za kulevya na utoaji wa elimu ya jinsi ya
kuepuka matumizi ya dawa hizo nchini, bwana Fabian J.Mkingwa alipokuwa
akizungumza na Capital redio juu ya mada iliyohusu, ‘Juhudi zinazofanywa na
serikali pamoja na wadau mbalimbali kuzuia matumizi ya dawa za kulevya
zimefanikiwa?
Katika maelezo yake hayo alitilia mkazo sana katika elimu ya
kijamii, ustawi wa jamii katika watu kujitambua. Alisema, “Mtu anapaswa kujitambua aweze kufahamu , ‘mimi kama mimi ninatakiwa kuwa nani siku za
usoni, nitatakiwa nipitie hatua zipi ili
kuwa kama hivyo ninavyotaka kuwa’.
Lakini pia kutengeneza jamii ya watu ambayo wanapenda kuthamini mafanikio
yaliyotokana na hatua halali za kufanikiwa.
Ikionekana kwamba tunamthamini mtu ambaye hatujui fedha kazipataje,
tujue kabisa mwisho wa siku watu watamuangalia yule na wengine watafuatilia amepataje
mafanikio. Sasa kama amepata mafanikio kwa kuuza madawa ya kulevya , maana yake
tutazalisha wauzajiwa dawa za kulevya wengi . Kwa hiyo sisi tutengeneze
mazingira ya kuwachukia, kutokuwakubali, hawa wanaofanya biashara ya dawa za kulevya, hata Misikitini,
Makanisani na kwingineko. Kama kuna mtu tunahisi ya kwamba anafanya biashara ya
dawa za kulevya, hata kama ana mafanikio
makubwa kiasi gani, tunahitaji fedha zake, sasa tuzikatae hizo fedha zake na
tusimthamini kwa sababu ya fedha zake.
Akidharaulika huyu, inawezekana kabisa kwamba tukatengeneza
kizazi cha vijana ambao wanajua kwa
kujiingiza katika biashara kama hii watadharaulika”
Bwana Fabian pia amesema kwamba Taasisi yao imeanzisha
kampeni iitwayo ‘ACHA KULALAMIKA’ ambayo inalenga kuifanya jamii, ikiwemo
serikali yenyewe kuacha kulaamika na kulaumiana kila kitu na badala yake kila
mtu atImize wajibu wake katika kutokomeza matatizo mbalimbali likiwemo hili la
dawa za kulevya.
0 Response to "“TUWAKATAE HAWA WAUZA UNGA MAKANISANI, NA MISIKITINI …”"
Post a Comment