Uruasi kupitia waziri wake wa mambo ya ndani Sergey Lavrov
ameiasa Syria kuharibu silaha zake za kikemikali ili kuizuia Marekani
isiishambulie.
Ingawa Urusi imekuwa ikikataa kukubali Serikali ya Syria kutumia Silaha hizo, lakini
baada ya Obama kuendelea kushikilia msimamo wake wa kuishambulia bila ya
kutetereka, sasa Urusi inaonyesha kulegeza msimamo wake.
Naye Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry
alipokuwa nchi za ulaya na kuulizwa ikiwa kuna lolote Syria inaweza kufanya kuepusha mashambulizi
alijibu kwamba, Syria inapaswa kukabithi shehena yake yote ya silaha za
kemikali kwa Umoja wa Mataifa ndani ya wiki moja.
0 Response to "URUSI YAISHAURI SYRIA KUSALIMISHA SILAHA ZA KEMIKALI"
Post a Comment