Arusha. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali,(PAC) Zitto Kabwe amesema kiasi cha Dola 2 bilioni za Marekani,
zinapotea serikalini kila mwaka kwa kutoroshwa nje ya nchi au katika ukwepaji
wa kodi .
Zitto alitoa taarifa hiyo jana, wakati akizungumza na waandishi
wa habari mjini Arusha.
Zitto, alisema hata hivyo tatizo hilo, si tu kwa Tanzania pekee
yake na kwamba taarifa za kimataifa zinaeleza kuwa kwa bara la Afrika , kiasi
cha Dola 700 bilioni zanatoroshwa nje ya bara kila mwaka.
Alisema fedha hizo ni zaidi ya misaada yote inayotolewa kwa nchi
za Afrika.
Chanzo ni Gazeti la Mwananchi.
0 Response to "‘Wajanja' wanatorosha Dola 2 bilioni"
Post a Comment