Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam
jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama,
wamepokea maombi kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki wa Injili nchini
wakiomba lifanyike katika mikoa yao.
![]() |
Alex Msama Mkurugenzi wa Msama Promotion na manzilishi wa Tamasha la Pasaka na Krismas |
Aliitaja
mikoa hiyo kuwa ni Mbeya, Mwanza, Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Shinyanga.
“Tunachofanya
kwenye kamati yangu ni kupokea maoni kwa njia mbalimbali ikiwemo simu za
mikononi kutoka kwa wadau wetu kwamba wapi wanataka tamasha lifanyike.
“Kwa
kipindi cha wiki moja tumepokea maombi mengi kutoka kwenye mikoa hiyo na kesho
(leo), ndiyo siku ya mwisho tuliyoweka kwa ajili ya kupokea maombi, baada ya
hapo tutatangaza mkoa gani utakuwa wa kwanza,” alisema Msama na kuongeza:
“Lakini si kupendekezwa tu na wadau ndiyo kigezo cha kupewa nafasi, lazima
tuangalie na mazingira ya mkoa husika katika mambo ya matamasha,” alisisitiza
Msama.
Tamasha
la Krismasi linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam,
ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.
Kwa
mujibu wa Msama wanataka Tamasha la Krismasi liwe bora zaidi kuliko la Pasaka
kwa kualika wasanii maarufu kutoka nje na ndani ya Tanzania.
Alisema
hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na tofauti
kubwa kulinganisha na matamasha mengine yaliyowahi kuandaliwa na kampuni yake.
Chanzo cha habari ni Tanzania Daima
0 Response to "MAANDALIZI YA TAMASHA LA KRISMASI, MIKOA SITA YATUMA MAOMBI"
Post a Comment