Kutoka
katika magazetini leo, Tanzania daima limeripoti kwamba mbunge viti maalumu CCM,
Rosweeter Kasikila anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 60 amefunga pingu za maisha
na kijana anayelingana na wanawe na aliyekuwa na umri wa miaka 26, Michael
Christian. Wanadaiwa kufunga harusi hiyo katika kanisa la TAG la Mchungaji kiongozi
Mama Getrude Lwakatare lililoko Mikocheni.
Hata hivyo
inadaiwa kwamba ndoa hiyo imeingia mgogoro uliopelekea wanandoa hao kuachana,
ambapo kijana huyo anayesoma katika chuo Kikuu cha Muhimbili, analalamika vyeti
vyake vya masomo na nyaraka zake nyeti kuzuiliwa na Mke wake huyo.
0 Response to "MBUNGE MWANAMKE MIAKA 60 AFUNGA NDOA NA 'MWANAWE' MIAKA 26"
Post a Comment