![]() |
Msichana akiwa maziwa wazi, nusu uchi |
Bi Clare Short,
aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza na Mbunge wa jimbo la Birmingham amesema kwamba ,vitendo vya
udhalilishaji wa wanawake kupitia picha chafu za ngono na nusu uchi katika
vyombo vya habari hususani magazeti sasa vimepungua kwa kiasi kikubwa kufuatia
kampeni yake na wanawake kwa ujumla waliyoianzisha tangu miaka ya 80, ijapokuwa
lakini ule ukurasa maarufu katika gazeti la the sun unaochapisha picha ya
msichana aliye nusu uchi, kifua na maziwa vyote vikiwa nje haujapigwa marufuku.
Alikuwa akizungumza na BBC kati kati ya jiji la
London yalipo makao makuu ya bbc kwenye Tamasha kubwa la wanawake 100,
lililoandaliwa na bbc yenyewe kwa mwezi mzima wa oktoba kwa ajili ya kuangazia
maswala mbalimbali yahusuyo kinamama na watoto wa kike kwa ujumla katika tasnia
nzima ya habari.
Tangu mwaka 1986, Bibi Short amekuwa katika
vita kali dhidi ya magazeti , hususan gazeti maarufu la udaku la THE SUN juu ya
ukurasa maarufu uliozua gumzo kubwa ujulikanao kama “Page 3” Ukurasa wa 3 ambao
hutoa picha kila toleo ya msichana kigoli aliyevaa nusu uchi, akiacha sehemu
yote ya juu uchi kuanzia kiunoni, maziwa
na kifua vyote vikiwa wazi.
Alifikia hatua ya kuwasilisha mswada bungeni
kutaka itungwe sheria ya kupiga marufuku kurasa kama hizo lakini kwa bahati
mbaya juhudi zake ziligonga mwamba pale spika alipoukataa. Hata hivyo nje ya
Bunge Gazeti lenyewe la The Sun liliendesha kampeni kali dhidi yake ya
kumdhalilisha na kumdhihaki, kwa mfano katika ukurasa huo wa 3 waliweka picha
ya Short ikimuonyesha mnene, na kisha wakaweka maandishi, “A VERY FAT PAGE 3
GIRL” Walituma waandishi nyumbani kwake wakamuwinde usiku na mchana ili kumpiga
picha za kumdhalilisha hata mbele ya mama yake mzee aliyekuwa na umri zaidi ya
miaka 80.
Chanzo, The Independent
Chanzo, The Independent
0 Response to "PICHA ZA NGONO NA NUSU UCHI ZIMEPUNGUA MAGAZETINI"
Post a Comment