![]() |
Mkuu wa huduma ya VHM, Mchungaji Mitimingi akitoa semina |
Katika
semina za vijana zinazotolewa kila mwezi
na Wapo Mission katika ukumbi wa BCIC Mbezi Beach maarufu kama semina za kuwaridhisha vijana vipawa
na maadili chini ya Askofu Sylvester Gamanywa, semina ya mwezi
huu, walialikwa wazungumzaji mbalimbali na miongoni mwao alikuwa ni Mchungaji
Peter Mitimingi wa huduma ya VHM aliyetoa
mada juu ya Mahusiano.
Katika
hotuba yake, aliwaasa vijana kujiepusha na ‘Mashugamami’ na ‘Mashugadady’ ili kujitegemea kimaisha. “Piga kazi kwa
mikono yako , Biblia inasema, Mungu atabariki kazi ya mikono yenu, siyo kazi za
mikono ya ile mijimama kule”. Alisema.
![]() |
Askofu Sylvester Gamanywa akiongea na vijana. |
Naye
Mzungumzaji mwingine, Dr. Binagwa akitoa mada alisema, “Ni vigumu sana kijana tunayemtaka
mwenye muelekeo mpya, mabadiliko mapya, mtazamo mpya, kama hana malengo
maishani, anajiendea, kama hafuati muda, kama hana imani, kama hajali, kama
hana nidhamu, kama hajengi uchumi binafsi, ni vigumu sana kijana huyo kuendelea”
Picha kutoka mitandao ya martamalecela.blogspot na wapofm.org
0 Response to " “VIJANA JIEPUSHENI NA MASUGARMUMMY NA MASUGARDADDY”: PASTOR MITIMINGI"
Post a Comment