Nyumba ya Diamond Platnumz katika pozi tofauti |
Baada
ya kuzungumza yanayomhusu katika kipindi cha ‘Take one’ cha Clouds TV, Diamond Platnumz
ameposti kwenye ukurasa wake wa Instagram picha ya nyuma yake anayojenga.
Diamond
ambaye katika mahojiano hayo na mtangazaji Zamaradi Mketema alisema thamani ya
nyumba hiyo hivi sasa ni zaidi ya shilingi billioni moja, ameposti picha ya ‘bangaluu’
lake jipya na ujumbe muhimu kwa wapenda starehe, “Toa kitu weka kitu…! Ndivyo tulivyofunzwa…starehe
tunawaachia wajanja wa mjini….Wasafi for the …life!” aliandika ujumbe huo wa
kuhamasisha kuwekeza ya badala ya kuponda tu maisha.
“Mi
naiogopa sana kesho ndiyo maana nawekeza. Kila pesa ninayopata nakata asilimia
ngogo sana kwa ajili ya matumizi muhimu na nyingine naweka benki” alisema
Diamond kumwambia Zamaradi. Nyota huyo wa Ngololo Dance pia aliifananisha gari
yake ya Toyota Prado aliyosema ameinunua kwa sh. Milion 59 kuwa ni sawa
makubadhi.
“Nilikuwa
nina pesa za kutosha wakati nainunua ile Prado, kuna wengine walisema kwanini
unachezea pesa , unatoa kiasi chote hicho, lakini ukweli ni kwamba wakati
nainunua nilikuwa na pesa hivyo ilikuwa ni sawa na nimeenda kununua sendos tu”
alisema Diamond.
Wanaomfuatilia
kwenye ukurasa wake wengine walimpongeza
lakini mmoja aliandika “Hiyo ni nyumba ya kawaida mno, kwa pesa nyingi
ulizokuwa nazo”
Chanzo cha picha: Teamtz .com
0 Response to "DIAMOND PLATNUMZ ATOA SOMO LA UWEKEZAJI BAADA YA KUONYESHA MJENGO WAKE"
Post a Comment