Katika makala zilizopita tumeangalia umuhimu wa kuwa na Website. Pia
tumeangalani hatua muhimu za kupitia mpaka
unakuwa na website. Lengo la website ni kufanya kazi na siku ya
mwisho wewe kama mmiliki ni lazima uone matokeo ya kazi iliyofanywa na website.
Ingawa kumekuwa na
mijadala sana kwenye uwanja wa IT juu ya upimaji wa matokeo ya IT, wengi
wakisema, ni ngumu kupima matokeo yanayosababishwa na IT pale ambapo IT inakuwa
ni muwezeshaji, na website ikiwa ni sehemu moja wapo. Ukweli ni kuwa, kwa
sasa IT si muwezeshaji tena, bali ni sehemu ya kazi. Hivyo, inatakiwa itoe
matokeo tena yanayopimika, na website ni sehemu mojawapo. Na lazima ijumuishwe
kwenye malengo ya kampuni / shirika.
0 Response to "JINSI YA KUPIMA MAFANIKIO YA WEBSITE YAKO - SEHEMU 1"
Post a Comment