Hospitali ya Millpark ya Johannesburg, Afrika Kusini, imesema
madaktari waliokuwa wakimtibu aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Dk Sengondo Mvungi walibaini kuharibika kwa ubongo wake kutokana na
kumwagika kwa maji yanayoutunza ambayo kitaalamu yanaitwa ‘cerebrospinal
fluids’ au CCF.
Msemaji wa Hospitali hiyo, Tebogo Nyembezi alisema Dk Mvungi alicheleweshewa tiba baada ya kupata tatizo la maji hayo yanayotunza ubongo kumwagika mara baada ya kujeruhiwa.
Dk Mvungi (61), alipata majeraha makubwa baada ya kujeruhiwa na
watu waliovamia nyumbani kwake Kibamba, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam,
Novemba 3 mwaka huu. Alifariki dunia jana mchana.
“Maji hayo ambayo ni miligramu 50 tu katika ubongo wa mwanadamu
ambayo huufanya ubongo uelee yakimwagika nusu tu, basi mgonjwa yupo hatarini,
lakini akiwahishwa na kupata tiba sahihi anaweza kupona,” alisema Nyembezi.
Alisema iwapo mgonjwa atapewa tiba sahihi ndani ya saa 48,
ubongo wake unaweza kurudi katika hali ya kawaida, lakini saa hizo zikizidi
hawezi kupona kabisa kwa sababu maji hayo yanapomwagika ubongo hujigonga kwenye
mifupa ya sakafu yake na kuharibika kabisa.
Mtaalamu wa mishipa na neva za fahamu (neurosurgeon) katika
Hospitali ya Regency, Dar es Salaam, Dk Hariff Najin alisema kazi kubwa ya maji
hayo ni kuulinda ubongo pindi inapotokea ajali ili usidhurike lakini endapo
maji hayo yatamwagika nao huharibika.
“Haya maji yanaufanya ubongo uelee na usielemee kichwa. Hivyo
inapotokea maji haya yakaisha au kupungua, ubongo hujigonga na kukosa ukinzani na
kuharibika,” alisema. Soma zaidi habari hii katika tovuti ya Mwananch hapa
0 Response to "Kilichomuua Dk Mvungi"
Post a Comment