Kipa namba moja nchini Tanzania Juma Kaseja akisaini mkataba wa kuichezea Yanga kwa kipindi cha miaka 2 huku mwenyekiti wa kamati ya mashindano Bin Klebl akishuhudia. |
Mlinda mlango nambari moja nchini Tanzania kwa kipindi
kisichopungua miaka 10 mfululizo Juma Kaseja Juma jana majira ya saa 2 usiku
alisaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Young Africans yenye makao yake
Twiga/Jangwani kwa kipindi cha miaka miwili.
Usajili wa Juma Kaseja kujiunga na klabu ya Yanga unafuatia
mapendekezo ya benchi la ufundi katika ripoti waliyoikabidhi kwa kamati ya
mashindano kwa ajili ya kuboresha kikosi kwa ajili mzunguko wa pili na
mashindano ya kimataifa.
Benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Ernie Brandts lilihitaji
mlinda mlango mwenye uzoefu wa michezo ya kimataifa kwa ajili ya kujiandaa na
michezo ya kimataifa na mzunguko wa pili ambao utakua na upinzani kulingana na
kila timu kutaka kufanya vizuri.
Akiongea na www.youngafricans.co.tz mara
baada ya kumalizika kwa zoezi hilo mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya
Yanga Abdallah BinKleb alisema hawana shaka na uwezo wa Kaseja kwani rekodi
yake ndani na nje ya nchi inafahamika kwa hiyo wanaamini atatoa mchango mkubwa
wa timu ya Yanga.
Timu yetu imekamilika kila idara, kikubwa tunachokifanya ni
kuhakikisha tunazidi kukiboresha na kuyafanyia kazi mapendekezo ya benchi la
ufundi ili kuhakikisha Yanga inaendelea kufanya vizuri na kutisha katika Ligi
Kuu ya Vodacom na mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
"Najua wegine watajiuliza maswali mengi kwa nini Yanga
wamemsajili Kaseja, ukweli ni kwamba walinda mlango waliopo ndani ya Tanzania
Kaseja bado ana uwezo nkubwa na msaada ambao atautoa katika kukiimarisha kikosi
chetu" alisema Bin Kleb
Kaseja hakua na timu yoyote aliyoichezea katika mzunguko wa kwanza
wa Ligi Kuu kufuatia kumalizika kwa mkataba wake na timu yake ya zamani ya
Simba SC hivyo kujiunga na Yanga kama mchezaji huru katika kipindi hichi cha
drisha dogo la usajili.
Kutua kwa Kaseja kunaifanya Yanga kuwa na walinda mlango wanne
wote wenye uwezo wa hali ya juu na kutokuwa na shaka wakati wowote timu
inapokuwa inakabaliana na mashindao yoyote iwe ni ndani ya nchi au ya nje ya
nchi (kimataifa).
Kaseja anaungana na walinda mlango wengine Ally Mustapha
'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul ambao wataitumikia klabu
ya Yanga kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom januari 2014 na
mashindano ya klabu Bingwa Afika 2014.
0 Response to "KIPA NAMBA MOJA TANZANIA JUMA KASEJA AANGUKA SAINI JANGWANI"
Post a Comment