Manusura wa Tufani kubwa na ambalo halijawahi kutokea katika
historia ya visiwa vya Ufillipino, Haiyan au ‘Yolanda’ kama wenyeji
wanavyoiita, wameilinganisha tufani hiyo na mwisho wa Dunia.
Kimbunga hicho
kilichosababisha uharibifu wa kutisha tayari kinahofiwa kuangamiza maisha ya
watu wapatao elfu kumi, wengi wakiwa ni wakazi wa mji mmoja peke yake uitwao
Tacloban.
Kwa mujibu wa shirika la
habari la BBC, majengo yote yameharibiwa vibaya, matope yametapakaa kila kona,
na harufu mbaya ya miili ya watu na mifugo iliyooza ndiyo iliyotawala.
Tayari Rais wa visiwa hivyo Benigno Aquino ametangaza hali ya
dharura huku akiiomba jumuiya ya Kimataifa kuwasaidia ili wahanga ambao hawana
chochote waweze angalao kupata maji chakula na malazi.
Wakati huo huo huko Nchini
Somalia katika jimbo la Puntland inaarifiwa kuwa watu wapatao mia moja wamekufa
kutokana na gharika iliyopiga huko mwishoni mwa wiki.
0 Response to "KIMBUNGA YOLANDA (HAIYAN) NI KAMA MWISHO WA DUNIA"
Post a Comment