Jackline Wolper 'Diva wa filamu Bongo' |
Masanja Mkandamizaji asema, Pesa haziijanisahaulisha dhiki na
Wolper kubadili imani kutoka Uislamu na kurudi Ukristo ni baadhi tu ya habari
zilizochukua uzito katika moja ya magazeti ya leo hii Jumatano ambalo ni SANI.
Staa huyo wa kundi la vichekesho la Original Komedi, Emmanuel
Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji amefunguka na kukiri kuwa kwa sasa anao
uwezo mkubwa kimaisha ingawa haumfanyi akasahau shida alizopitia na ambazo
jamaa aliosota nao kipindi cha nyuma wanazipata.
Masanja amesema kwamba usanii umemfanya kumiliki mjengo wa kisasa na
magari kadhaa ambapo ana uwezo wa kubadili mboga lakini hakuna anachoogopa kama
kufilisika na kurudi tena kwenye umasikini.
Naye nyota mwingine katika maswala ya filamu mwanadada
Jackline Wolper, ‘Diva wa filamu Bongo’ anadaiwa kubadili imani yake ya dini ya
kiislamu na kurudia Ukristo dini
aliyokuwa zamani kabla ya kusilimu. Inasemekana na marafiki zake wa karibu
kwamba siku ya Jumapili alionekana katika kanisa moja la KKT huko Kijitonyama
huku akiwa ameshikilia biblia mkononi.
Kwa habari hizo kwa undani na nyinginezo nyingi za
kusisimua, tafadhali jipatie nakala ya gazeti lako la SANI Burudisho la
Wasomaji siku ya leo tarehe 6 Novemba 2013.
0 Response to "MASANJA MKANDAMIZAJI: PESA HAZIJANISAHAULISHA DHIKI, WOLPER ARUDIA TENA UKRISTO AACHA UISLAMU"
Post a Comment