Mwanafunzi wa kidato cha nne
ambaye ni mtahiniwa mwaka huu wa 2013,
Simon Kahamba (18) amebambwa na askari wanaolinda mitihani hiyo, baada ya
kumshitukia akiwa tayari ameshabinjukia ndani ya chumba cha kuhifadhia mitihani
kwa lengo la kuiba ‘paper’ mtihani wa kemia.
Tukio hili lilitokea jana
Wilayani Shinyanga vijijini katika shule
ya sekondari Ibisera, iliyopo katika Tarafa ya Ibisera baada ya askari kumkuta
mwanafunzi huyo tayari amekwisha vunja kufuli moja la kabati la kuhifadhia
mitihani hiyo ya Taifa. Askari walipomhoji alisema yeye hamu yake kubwa ilikuwa ni ‘paper
ya kemia’, mtihani wa chemistry pekee, aliokuwa akitamani kuuiba.
Uchunguzi wa tukio hili
unaendelea na Kaimu kamanda wa polisi wilayani humo Kamanda Keenye ameiambia Radio
Free Afrika kuwa mtahiniwa huyo wa kidato cha nne atafikishwa mahakamani mara
tu uchunguzi utakapokamilika.
0 Response to "MTAHINIWA FORM IV AVUNJA CHUMBA CHA MTIHANI AKITAKA KUIBA PAPER YA KEMIA"
Post a Comment