Bi Jone katikati |
Mwanamke, aliyezaliwa mwaka
1899 tarehe 7 Disemba, karne ya 19, Miss Jones amefariki dunia akiwa na umri wa
miaka 113. Aliishi katika jiji la London kitongoji kiitwacho Bermondsey, na
alikuwa akishikilia namba sita katika orodha ya watu wenye umri mkubwa zaidi
wanaoishi duniani kwa sasa. Baada ya afya yake kuanza kudorora siku za hivi
karibuni alilazwa katika Hospitali ya St.Thomas
ambayo ndiyo hospitali alikolazwa Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu
Julius Kambarage Nyerre kabla hajafariki dunia hapo mwaka 1999.
Jirani yake mmoja aitwaye
Hughes anasimulia kwamba, hadi kifo chake Bi Jones alikuwa na akili timamu tena
hakuonyesha kabisa kuhofia kifo na anasema pia kwamba alishiriki katika vita
kuu ya 1 ya Dunia na mchumba wake alikufa akiwa anahudumu katika vita hiyo.
Alikuwa akiishi ghorofani katika chumba chake mwenyewe na mpaka siku za hivi
karibuni alikuwa akifanya shopping mwenyewe sokoni.
Majirani zake wote na
marafiki wanaelezea kusikitishwa sana na kifo chake na wanasema kamwe
hawatamsahau. Kifo cha Bi Jones kina maanisha kwamba kwa sasa mtu mzee kuliko
wote nchini Uingereza ni Ethel Lang kutoka Barnsley aliyezaliwa mwezi wa 5 mwaka 1900. Ina maana kwamba Bi Jones ni
mtu wa mwisho aliyezaliwa miaka ya 1800 au karne ya 19 kufariki dunia.
Alizaliwa Karne ya 19, akaishi Karne ya 20 na amefariki Karne ya 21. Mungu ailaze
roho yake Mahala pema peponi Amen.
0 Response to "MTU WA SITA MZEE KULIKO WOTE DUNIANI AFIA HOSPITALI ALIYOFIA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE, AMEISHI NA KUSHUHUDIA KARNE ZOTE 3 "
Post a Comment