![]() |
Picha hii ya mtandaoni (mfano) ikimuonyesha Kaini alivyokuwa akimuua ndugu yake Abel kwa wivu |
Kisa
kilichowastaajabisha watu wengi na kinachofanana kwa asilimia kubwa na kile
kisa maarufu katika misahafu ya dini ikiwemo Biblia Takatifu cha Kaini na Abel
kimetokea huko Wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya baada ya msichana mdogo,
Faraja Itika mwenye umri wa miaka 14
pekee na anayesoma Shule ya sekondari Mwakyusi katika kijiji cha Ipelo kumuua dada yake, Pendo Abel mwenye umri wa miaka 28 kutokana na sababu ya
kumuonea wivu baada ya kuvuna mazao mengi ya viazi kumshinda ambapo mashamba
yao yamepakana.
Faraja
alimfuata dada yake shambani alikokuwa akivuna viazi kisha kwa kutumia kisu
akamchoma shingoni na kufariki dunia palepale. Faraja alikuwa peke yake lakini
baadhi ya wapitanjia waliposhitukia tukio hilo ndipo walipoamua kumkamata na
walipomhoji alidai kwamba kila anapolima
mazao yeye hupata mazao kidogo wakati Pendo yeye hupata mazao mengi na hiyo
ndiyo sababu anayodai ilimsukuma kumuua dada yake.
Ndu
jamaa na marafiki wameshangazwa sana na tukio hili na wanasema linawatia aibu na
fedheha kubwaa katika ukoo wao ukizingatia kwamba umri aliokuwa nao Pendo ni
mara mbili ya ule aliokuwa nao Faraja isitoshe anategemewa na familia, wanasema
kitendo hicho kitaleta laana kubwa katika ukoo wao. Kaimu kamanda wa polisi
Mkoani Mbeya Robert Mayalla ametoa wito kwa jamii kutatua migogoro ya kifamilia kwa kukaa meza ya mazungumzo ili
kupata suluhisho badala ya kujichukulia sheria mikononi, pia amesema kwamba sheria itachukua mkondo wake dhidi ya Faraja licha ya umri wake kuwa
mdogo.
Katika
vitabu vya dini tunaambiwa kwamba Kaini alimuua ndugu yake Abel baada ya wivu
kama huo ambapo Mungu alipendezwa zaidi na sadaka alizotoa Abel hivyo kumbariki
akawa anapata mazao mengi shambani kwake. Kaini kuona vile chuki na hasira
zilimpanda akaamua kwenda kumuua kwa rungu na hapo ndipo Mwenyezi Mungu
alipomshushia Kaini laana kubwa zaidi katika uzao wake.
Chanzo cha stori ni Radio Wapo Fm, Patapata.
0 Response to "MWANAFUNZI FORM ONE AMUUA DADAKE KAMA ALIVYOFANYA KAINI KWA ABELI"
Post a Comment