Dar es Salaam. Afya za maelfu ya walaji wa nyama katika Jiji la Dar es Salaam zipo hatarini baada ya kubainika kuwa nyama inayochinjwa katika machinjio mengi haifai kwa matumizi ya binadamu.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika machinjio mbalimbali ya maeneo ya Vingunguti, Ukonga, Kimara Suka, Tegeta na Mbagala, umebaini taratibu za kuchinja hazifuatwi huku maeneo hayo yakiwa yamejaa uchafu.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika machinjio hayo kwa nyakati tofauti alfajiri na kushuhudia ukiukwaji wa taratibu za uchinjaji, ambapo nyama zinatupwa ovyo, kwenye mazingira hatari, huku nyingine zikiwekwa karibu na madimbwi ya maji machafu.Endelea kuisoma habari hii katika gazeti lako la Mwanachi hapa.
0 Response to "Nyama hatari yauzwa nchini"
Post a Comment