Dar es Salaam. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Fasihi ya Lugha, Profesa Ngugi wa Thiong’o kutokana na mchango wake mkubwa kwa Bara la Afrika katika kujikomboa kiakili dhidi ya ubeberu wa lugha za kigeni.
Ngugi ambaye ni nguli wa fasihi za lugha na pia ni mhadhiri
katika Chuo Kikuu cha California huko Marekani, alitunukiwa shahada hiyo jana,
Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya 43 ya UDSM.
Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema chuo
kimeamua kumpa shahada hiyo kutokana na mchango wake wa kupinga chuki na dharau
zinazofanywa na mataifa ya Ulaya dhidi ya lugha za Afrika.
“Katika jitihada hizo, Chuo Kikuu kimeruhusu tasnifu (Thesis) za
Shahada ya Uzamili na Uzamivu katika Kiswahili ziwasilishwe katika Lugha ya
Kiswahili. Pia Chuo kinasisitiza kuwa tasnifu zote hapa chuoni ziwe na
muhtasari mfupi ulioandikwa kwa Kiswahili,” alisema.
Akishukuru baada ya kukabidhiwa shahada hiyo , Ngugi alisema
hiyo ni shahada yake ya nane kutunukiwa na vyuo mbalimbali duniani na ya pili
kwa Afrika.
0 Response to "PROFESA NGUGI WA THIONG'O ATUNUKIWA UDAKTARI WA FASIHI UDSM"
Post a Comment