Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete (JK) |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo hii akihutubia Taifa
kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema kwamba Tanzania
haitajitoa katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki licha ya Baadhi ya Mataifa ya
Jumuiya hiyo hususan Kenya, Uganda na Rwanda kuonyesha dalili za kuitenga.
Alisema, “Kila siku tunasikia eti kuwa baadhi ya viongozi hao walipoulizwa,
kwa nini wenzenu hawapo, wakasema wao wametangulia tu lakini sisi wengine tutakapokuwa
tayari tutajiunga nao. Yuko mmoja akasema ‘coallision of the willing’ yaani umoja wa wale waliokuwa tayari, sasa
tunauliza, hivi nani hayuko tayari?. Rais aliongeza pia kwamba Tanzania
ina uzoefu katika maswala ya muungano kutokana na kuwa katika muungano wa
Tanganyika na Zanzibar.
Kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rais
Kikwete amempongeza Rais Joseph Kabila kutokana na kuwasambaratisha waasi wa
M23 na pia amesema jukumu kubwa
alilokuwa nalo Kabila sasa ni la kudumisha amani na kuziunganisha tena pande
zilizokuwa zikihasimiana.
Amezungumzia pia suala la ujangili na kukumbushia
operesheni iliyoanzishwa na serikali hivi karibuni ya kukabiliana na
majangili wa wanyamapori hasa Tembo na Faru, na amesema kwamba serikali
itaendelea na operesheni za mara kwa mara kumaliza tatizo hilo.
Rais Kikwete, hii ni mara yake ya pili kulihutubia
Bunge tangu aingie madarakani.
0 Response to "RAIS JK: TANZANIA HAITAJIONDOA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI"
Post a Comment