Rais wa 35 wa Marekani John F Kennedy aliyeuwawa kwa kupigwa risasi kichwani. |
“Raisi
wa Marekani John F Kennedy ameuwawa kwa risasi” Hayo ndiyo maneno yaliyosikika
kwenye Televisheni na radio nchini Marekani siku ya tarehe 22 Novemba mwaka 1963 mjini Dallas Texas karibu na jengo maarufu la Dealey
Plaza,dakika chache baada ya kijana mmoja mdunguaji aliyejulikana kwa jina la Lee Harvey Oswald kumlenga raisi huyo kichwani kwa risasi huku yeye akiwa juu ya
ghorofa.
Rais Kennedy wa 35 kuliongoza Taifa hilo lenye
nguvu duniani alikuwa ndani ya gari yeye na mkewe Jacqueline pamoja na Gavana
wa Texas John Connaly wakienda katika mkutano
kukutana na viongozi mbalimbali wa kiraia na kibiashara katika mji wa
Texas, na yeye pamoja na makamu wake wa Rais Lyndon Johnson waliamua kutumia njia ya barabara kwa lengo la kuhamasisha wananchi
kujitokeza kwa wingi zaidi.
Muuaji Lee Harvey Oswald baadaye ilibainika na
tume ya Warren kwamba Muuaji alitekeleza
mauaji hayop peke yake pasipo kuhusika kikundi wala serikali yeyote kama
ilivyokuwa imedhaniwa na wengi kwamba huenda labda Urusi, na Cuba waliokuwa
mahasimu wakubwa wa Marekani walikuwa na mkono wao katika mauaji hayo.
Hata hivyo siku chache hata kabla ya muuaji
kufikishwa kortini kwa mashitaka ya uhaini mtu mwingine naye Jack Rubby mmiliki
wa klabu ya usiku, kutokana na uchungu wa kuuwawa kwa raisi wake naye aliamua
kwa kutumia risasi kumuua Lee Harvey Oswald wakati akipelekwa mahakamani huko
Dallas.Tukio hilo la kuuwawa muuaji wa Rais Kennedy lilikuwa likionyeshwa live
katika American Television.
Rais Kennedy ambaye jina lake kwa kirefu ni John Fitzgerald Kennedy ,alikuwa ndiye
Raisi aliyeingia madarakani akiwa na umri mdogo zaidi katika historia ya Taifa
la Marekani akiwa na umri wa miaka 43 pekee amemzidi Obama kwa miaka 4
aliyeingia madarakani mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 47. Alizaliwa mwaka 1917 tarehe 29 May na alichaguliwa kuliongoza Taifa la Marekani
mwaka 1961 tarehe 20 mwezi Januari mpaka pale alipouwawa.
Leo ni maka 50 tangu kuuwawa kwa Rais Kennedy
na maadhimisho yake yanafanywa katika eneo alipouwawa kwa umati wa watu
kukusanyika Dealey Plaza. Raisi Obama ameamrisha bendera nchini humo
kupeperushwa nusu mlingoti na kuuelezea utawala wa Kennedy kwamba ulikuwa
katika kipindi ambacho vita baridi kati ya Marekani na Urusi vilishamiri huku
Urusi ikiyapeleka makombora yake ya Nuklia katika visiwa vya Cuba enzi za
Castro, vile vile kilikuwa ndiyo kipindi mapambano ya Wamarekani weusi dhidi ya
ubaguzi wa rangi yalipokuwa yakipamba moto.
0 Response to "RAISI WA MAREKANI JOHN F KENNEDY ALIVYOUWAWA KWENYE MSAFARA"
Post a Comment